Ufalme : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 27: Mstari 27:
==Ukoloni na ufalme==
==Ukoloni na ufalme==
[[Ukoloni]] wa [[karne ya 19]] ulisababisha kupotea kwafalme nyingi dunani. Mwanzoni wakoloni walitumia mara nyingi wafalme na watemi waliokuwepo kama makala wa utawala wao ndani za koloni. Lakini kadri walivyounganisha falme mbalimali za kale ndani ya maeneo mapya makubwa yaliyoendelea kuwa mataifa mapya walidhoofisha pia nafasi ya ufalme wa kieneo. Nchi za [[Afrika]] zilipopata uhuru mara nyingi zilijitangaza kuwa jamhuri na kwa njia hii falme za kale za Afrika ama zilifutwa au kupoteza madaraka za kiutawala na kubaki kwa jina tu kama taasisi za kiutamaduni.
[[Ukoloni]] wa [[karne ya 19]] ulisababisha kupotea kwafalme nyingi dunani. Mwanzoni wakoloni walitumia mara nyingi wafalme na watemi waliokuwepo kama makala wa utawala wao ndani za koloni. Lakini kadri walivyounganisha falme mbalimali za kale ndani ya maeneo mapya makubwa yaliyoendelea kuwa mataifa mapya walidhoofisha pia nafasi ya ufalme wa kieneo. Nchi za [[Afrika]] zilipopata uhuru mara nyingi zilijitangaza kuwa jamhuri na kwa njia hii falme za kale za Afrika ama zilifutwa au kupoteza madaraka za kiutawala na kubaki kwa jina tu kama taasisi za kiutamaduni.
[[Picha:World Monarchies.png|thumb|300px|Nchi zenye mfumo wa ufalme<br> nyekundu: Ufalme bila masharti ya kikatiba; chungwa: ufalme chini ya masharti kiasi ya kikatiba; kijani: ufalme wa kikatiba; kijani kibichi: nchi za [[Jumuiya ya Madola]] chini ya malkia wa Uingereza; dhambarau: ufalme wa kieneo chini ya ngazi ya jamhuri ya kitaifa]]
[[Picha:World Monarchies.svg|thumb|300px|Nchi zenye mfumo wa ufalme<br> nyekundu: Ufalme bila masharti ya kikatiba; chungwa: ufalme chini ya masharti kiasi ya kikatiba; kijani: ufalme wa kikatiba; kijani kibichi: nchi za [[Jumuiya ya Madola]] chini ya malkia wa Uingereza; dhambarau: ufalme wa kieneo chini ya ngazi ya jamhuri ya kitaifa]]


==Ufalme leo==
==Ufalme leo==

Pitio la 04:00, 28 Aprili 2011

Taji la mfalme Louis XV wa Ufaransa; taji ni alama za cheo cha mfalme katika nchi nyingi

Ufalme ni mfumo wa utawala ambako mfalme, malkia au mtu mwingine aliyerithi cheo chake ni mkuu wa dola. Vyeo vingine vya mkuu katika ufalme ni pamoja na kaisari, shah, tenno, sultani, amiri au mtemi. Kwa kawaida mfalme amerithi cheo chake kutoka kwa babake au mamake kwa hiyo alizaliwa kama mfalme mteule na ataendelea kuwa na cheo hiki hadi kifo chake. Lakini kama mfalme aliyetangulia hakuwa na mrithi inawezekana ya kwamba mfalme mpya amechaguliwa. Mfano wa dola lenye mfumo wa ufalme ambako mkuu anachaguliwa mara kwa mara ni Vatikani ambao Papa ni mkuu wa dola.

Neno ufalme hutumiwa pia kwa kutaja nchi inayotawaliwa na mfalme au malkia, kwa mfano Ufalme wa Maungano, Ufalme wa Uswazi na kadhalika.

Kiwango cha madaraka cha mfalme huwa na tofauti kubwa. Leo hii karibu wafalme wengi wako chini ya katiba ya nchi na mara nyingi wana madaraka machache; nafasi yao ni ya heshima na desturi. Lakini kuna falme kadhaa ambako mfalme bado ana madaraka makubwa habanwi na katiba wala bunge wala serikali kama vile Omani au Saudia.

Tofauti ya ufalme na jamhuri

Kinyume cha ufalme ni jamhuri inayoongozwa na mkuu, mara nyingi kwa cheo rais au katika nchi kadhaa na kamati ya watu wanaochaguliwa na kwa kawaida kwa kipindi fulani. Mara nyingi rais wa nchi huchaguliwa kwa kipindi cha miaka 4-6 na katika nchi nyingi kuna uwezekano ya kwamba anarudi tena kwa kipindi cha ziada. Kuna jamhuri ambako vongozi wanalenga kuhakikisha ya kwamba mtoto wao anaendelea na cheo cha mkuu wakiacha kutawala lakini hii kwa kawaida si utaratibu wa kisheria katika jamhuri; mfano wa kisasa ni Korea Kaskazini ambayo ni jamhuri inayotawaliwa na familia Kim katika kizazi cha pili ilhali mtoto wa kiongozi Kim Jong Il anateuliwa kumfuata baba.

Historia

Sababu za kuanzishwa kwa ufalme

Ufalme ni muundo wa kale sana lakini haikuwa mfumo wa kwanza wa serikali. Wataalamu huona ya kwamba chanzo chake ni azimio la kabila au kundi dogo la watu kumruhusu mtoto wa kiongozi mwenye nguvu na uwezo kuendelea na shughuli za baba. Kuna mifano ya kwamba watu walioishi na viongozi wa muda tu waliamua kuwa na mfalme wakati wa vita wakiona uongozi mwenye nguvu ni lazima. Kulitokea pia ya kwamba kiongozi aliyeteuliwa kwa kipindi cha matatizo au vita alionekana kuwa na uwezo akaendelea hadi kifo na kumpatia mtoto wake nafasi ya mrithi wakati bado alikuwa na nguvu.

Historia ya Biblia kama mfano wa kuanzishwa kwa ufalme

Biblia inasimulia mfano jinsi gani watu wa Israeli ya Kale walioongozwa kila mahali na wazee lakini kama walipata matatizo makubwa viongozi walijitokeza walioitwa "maamuzi" na kuwa na jukumu za kijeshi pamoja na kisheria. Kitabu cha Maamuzi 8#22 kinaonyesha pia jinsi gani swali la ufalme lilikua na ugumu; mwamuzi Gideon alipoombwa na watu kuwa mfalme alikataa na kudokeza ya kwamba Mungu pekee anastahili kuwa na cheo hiki. Baadaye Sauli alijitokeza kama kiongozi dhidi ya tishio la Waamoni alipowashinda vitani watu walimfanya Sauli mfalme wao wa kwanza. Mataifa mengi walipata ufalme kwa njia zilizofanana na Israeli ya Kale yaani wakati wa vita ambako wengi walikubali haja la kiongozi mwenye nguvu.

Kupinduliwa kwa wafalme au kubanwa kwa madaraka yao

Mfano mashuhuri wa kinyume ni historia ya Athens au Roma ya Kale ambao zilitawaliwa zamani na wafalme lakini viongozi wa miji hii walifukuza wafalme baada ya kuona tabia za kidikteta na upuuzi wa haki za watu na kuanzisha jamhuri zilizoteuliwa na viongozi waliochaguliwa kwa muda tu. Lakini Roma ya Kale ilirudi kwa mfumo wa ufalme tangu Kaisari Augusto ingawa kwa jina iliendelea kama jamhuri hadi mwisho.

Mara nyingi wafalme waliunganisha nafasi za mkuu wa serikali na kiongozi wa jeshi na jaji mkuu. Mataifa mbalimbali walimjua mfalme pia katika nafasi ya kidini kama kuhani mkuu au kama mkuu anayeshika nafasi ya Mungu duniani.

Mamlaka makubwa ya wafalme yalisababisha mara nyingi jitihada za kubana madaraka yao. Mfano mashuhuri ni Uingereza ambako wafalme walipaswa kushauriana na bunge ya wakubwa na wawakilishi wa miji kabla ya kukusanya kodi kwa ajili ya vita au kwa shughuli maalumu. Jmabo kama hili halikutokea katika Uingereza pekee lakini katika nchi hii bunge lilikuwa taasisi ya kudumu isiyofutwa tena na hivyo kuwa chanzo kwa muundo wa ufalme wa kikatiba ambako mamlaka ya mfalme yako chini ya sheria fulani.

Tangu uhuru wa Uholanzi, Marekani na baadaye mapinduzi ya Kifaransa nafasi ya ufalme ilianza kupungua katika Ulaya na kutoka hapa pia katika sehemu nyingine za dunia. Hasa baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia falme muhimu kama Ujerumani, Austria-Hungaria, Urusi na Milki ya Osmani zilibadilisha mfumo wa utawala zikawa jamhuri.

Ukoloni na ufalme

Ukoloni wa karne ya 19 ulisababisha kupotea kwafalme nyingi dunani. Mwanzoni wakoloni walitumia mara nyingi wafalme na watemi waliokuwepo kama makala wa utawala wao ndani za koloni. Lakini kadri walivyounganisha falme mbalimali za kale ndani ya maeneo mapya makubwa yaliyoendelea kuwa mataifa mapya walidhoofisha pia nafasi ya ufalme wa kieneo. Nchi za Afrika zilipopata uhuru mara nyingi zilijitangaza kuwa jamhuri na kwa njia hii falme za kale za Afrika ama zilifutwa au kupoteza madaraka za kiutawala na kubaki kwa jina tu kama taasisi za kiutamaduni.

Nchi zenye mfumo wa ufalme
nyekundu: Ufalme bila masharti ya kikatiba; chungwa: ufalme chini ya masharti kiasi ya kikatiba; kijani: ufalme wa kikatiba; kijani kibichi: nchi za Jumuiya ya Madola chini ya malkia wa Uingereza; dhambarau: ufalme wa kieneo chini ya ngazi ya jamhuri ya kitaifa

Ufalme leo

Kuna nchi 44 dunaini zilizoendela na mfumo wa ufalme hadi karne ya 21. (lnganisha jedwali). Ufalme wa kale ni Japani ambako kuna wafalme tangu zaidi ya miaka 2000. ni United Kingdom,where the present line of Kings and Queens has been around for nearly 1,000 years, Denmark where the royal line has remained unbroken for almost 1,200 years, and Japan, which has records showing a line of Emperors dating back even farther.

Nchi

Aina ya ufalme

Cheo

Jina

Maelezo

Japan Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge Tenno Akihito Tenno hana madaraka ya kisiasa. Tangu 1945 ni mwakilishi wa taifa pekee. Japani ni ufalme wa kale duniani tangu zaidi ya miaka 2500. Cheo cha tenno chamaanisha „mtawala wa kimbingu“
Antigua na Barbuda[1] Ufalme wa kikatiba - chini ya usimamizi wa bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
Australia[1]
Bahamas[1]
Bahrain Ufalme wa kikatiba Mfalme Hamad ibn Isa Al Khalifa Hadi 2002 Emirati, baadaye ufalme; tangu mabadiliko ya kisiasa imekuwa ufalme wa kikatiba
Barbados[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge- Malkia Elizabeth II wa Uingereza
Ubelgiji Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge Mfalme Albert II
Belize[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
Bhutan Ufalme wa kikatiba Mfalme Jigme Khesar Namgyel Wangchuck [[ 1907 hadi 18 Julai 2008 ufalme bila masharti, tangu 2008 ufalme wa kikatiba
Denmark Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Margrethe II Mfalme / malkia wa Denmark ni pia mkuu wa nchi ya Greenland na ya Visiwa vya Faroe.
Grenada[1] Elizabeth II wa Uingereza
Jamaika[1]
Jordan Ufalme wa kikatiba Mfalme Abdullah II nchi ilianzishwa 1921 na Ufalme wa Maungano
Kambodia Norodom Sihamoni hadi 1955 na tangu 1993 ufalme
Kanada[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
Ufalme wa Nchi za Chini (Uholanzi) Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge Beatrix I Ufalme unajumlisha Uholanzi katika Ulaya na majimbo ya kujitawala katima Amerika ya Kati Aruba, Curaçao na Sint Maarten.
Lesotho Mfalme Letsie III Mfalme aliitwa hadi 1965 „Mtemi Mkuu“. Mfalme hana madaraka ya kiserikali wala hatungi sheria
Malaysia Mizan Zainal Abidin Ufalme wa uchaguzi - Malaysia ina majimbo 13 na kati ya hizi usultani 9; mfalme huchaguliwa kila baada ya miaka 5 masultani 9 kati yao kwa njia ya kubadilishana nafasi; cheo cha mfalme ni Yang di-Pertuan Agong „mtawala mkuu“
Moroko Ufalme wa kikatiba Mohammed VI
New Zealand[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
Norwei Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge Mfalme Harald V Ufalme wa kujitegema tangu 1905.
Papua Guinea Mpya[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
Visiwa vya Solomon[1]
Uarabuni wa Saudia Ufalme bila masharti Mfalme ʿAbd Allah ibn ʿAbd al-ʿAziz Ufalme wa Kiislamu uliounganshwa 1931
Uswidi Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge Carl XVI Gustaf
Hispania Juan Carlos I Ufalme hadi 1931; tena tangu 1947 chini ya dikteta Franco bila mfalme na tangu 1975 chini ya mfalme Juan Carlos
St. Kitts na Nevis[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
St. Lucia[1]
Saint Vincent na Grenadini[1]
Uswazi Ufalme bila masharti Mfalme Mswati III. Harakati ya kidemokrasia iko njiani
Uthai Ufalme wa kikatiba Bhumibol Adulyadej (Rama IX)
Tonga George Tupou V
Tuvalu[1] Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge malkia Elizabeth II wa Uingereza
Ufalme wa Maungano Malkia wa Uingereza ni pia mkuu wa nchi kwa „maeneo chini ya taji la Uingereza“ ambayo ni Guernsey, Jersey, Isle of Man halafu kwa maeneo ya ng’ambo ya Ufalme wa Maungano kama vile:, Anguilla, Bermuda, Visiwa vya Virgin vya Uingereza, Eneo la Uingereza katika Bahari Hindi, Visiwa vya Cayman, Visiwa vya Falkland, Gibraltar, Montserrat, Visiwa vya Pitcairn, Saint Helena, Visiwa vya South Georgia na South Sandwich na Visiwa vya Turks-na Caicos.
Utemi
Luxemburg Ufalme wa Kikatiba – chini ya mamlaka ya bunge Mtemi Mkubwa Henri I
Andorra Ufalme wa kikatiba - mamlaka ya bunge Watawala wa pamoja Askofu Joan Enric Vives i Sicília Andorra ina watawala wawili wenye madaraka na heshima ya pamoja ambayo ni askofu wa Urgel (Hispania) na Rais wa Ufaransa
Nicolas Sarkozy
Liechtenstein Ufalme wa kikatiba Mtemi Hans Adam II
Monaco Albert II
Usultani na Emirati
Brunei Ufalme bila masharti Sultani Hassanal Bolkiah
Oman Qabus ibn Said
Katar Ufalme bila masharti Emir Hamad bin Chalifa Al Thani
Kuwait Ufalme wa kikatiba Sabah al-Ahmad al-Dschabir as-Sabah Hadi 1991 ufalme bila masharti, tangu 1996 ina bunge
Falme za Kiarabu Shirikisho-Ufalme wa kikatiba Rais Chalifa bin Zayid Al Nahyan Ufalme wa uchaguzi: kuna emirati 7; kila emir angeweza kuchaguliwa kuwa rais wa shirikisho lakini hadi sasa ni Emir wa Abu Dhabi ambayo ni sehemu kubwa na tajiri aliyechaguliwa kila safari.
Eneo la Vatikani
Vatikani Ufalme bila masharti Papa Benedikto_XVI Ufalme bila masharti wa mwisho katika Ulaya; Papa huchaguliwa na mkutano wa mkardinali
  1. 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 1.12 1.13 1.14 Nchi ya Jumuiya ya Madola ambako malkia ya Uingereza ni mkuu wa dola anayewakilishwa na gavana mkuu