Njia Nyeupe : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
masahihisho
Mstari 10: Mstari 10:
== Kuonekana kwa Njia Nyeupe kutoka duniani ==
== Kuonekana kwa Njia Nyeupe kutoka duniani ==


[[Nyota]] karibu zote zote tunazoona kwa macho yetu wakati wa usiku ni sehemu za Njia Nyeupe. Wakati wa giza tunaweza kuona kati ya nyota 3,000 hadi 5,000 kwa macho yetu bila msaada wa [[hadubini]]. Isipokuwa [[sayari]] chache za jua letu na [[kometi]] (zinazoonekana mara chache tu) nyota zote ni majua kama jua letu. Si rahisi kuona nyota nyingi tukiwa mjani penye nuru nyingi wakati wa usiku kwa sababu mwanga wa taa za mjini unaakisiwa katika [[angahewa]] na kuleta matata ya kuona mwanga kutoka nje ya angahewa.
[[Nyota]] karibu zote zote tunazoona kwa macho yetu wakati wa usiku ni sehemu za Njia Nyeupe. Wakati wa giza tunaweza kuona kati ya nyota 3,000 hadi 5,000 kwa macho yetu bila msaada wa [[darubini]]. Isipokuwa [[sayari]] za jua letu na [[kometi]] ''(zinazoonekana mara chache tu)'' na [[galaksi ya Andromeda]] ''(inayoonekana kama nyota 1)'' nyota zote ni majua kama jua letu. Si rahisi kuona nyota nyingi tukiwa mjini penye nuru nyingi wakati wa usiku kwa sababu mwanga wa taa za mjini unaakisiwa katika [[angahewa]] na kuleta matata ya kuona mwanga kutoka nje ya angahewa.


Nyota zilizo nyingi kabisa hatuwezi kuziona wala kubainisha kwa hiyo zinatokea machoni kama ukungu mweupe tu.
Nyota zilizo nyingi za Njia Nyeupe hatuwezi kuziona wala kubainisha kwa hiyo zinatokea machoni kama ukungu mweupe tu.


Uwezo wetu kuona nyota nyingi umepungukiwa na kuwepo kwa [[mavumbi ya kinyota]] kati ya mahali petu na kitovu cha galaksi.
Uwezo wetu kuona nyota nyingi umepungukiwa na kuwepo kwa [[mavumbi ya kinyota]] kati ya mahali petu na kitovu cha galaksi.

Pitio la 15:18, 25 Aprili 2011

Njia nyeupe jinsi inavyoonekana usikun (Mistari mekundu kuonyesha mipaka yake; sehemu ya chiniya picha inafichwa na mti
Galaksi yetu jinsi inaaminiwa kuonekana vile kama tunaiangalia kutoka juu; picha ya galaksi ya mbali yenye mikono miwili ya pafafujo

Njia nyeupe, pia majarra au "mkokoto wa kondoo za Sumaili" [1] ni jina kwa kanda la nyota nyingi inaloonekana wakati wa usiku angani kama wingu neupe linalong`aa.

Hali halisi hii ni jinsi tunavyoona galaksi yetu ambamo jua letu na mfumo wake ni sehemu yake.

Galaksi yetu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Umbo lake unafanana na kisahani chense umbo la parafujo. Kipenyo cha kisahani hiki ni miaka ya nuru 100,000 ikiwa na unene wa miaka ya nuru 3,000. Galaksi ya jirani iliyo karibu angani inaitwa Andromeda ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5 .

Kuonekana kwa Njia Nyeupe kutoka duniani

Nyota karibu zote zote tunazoona kwa macho yetu wakati wa usiku ni sehemu za Njia Nyeupe. Wakati wa giza tunaweza kuona kati ya nyota 3,000 hadi 5,000 kwa macho yetu bila msaada wa darubini. Isipokuwa sayari za jua letu na kometi (zinazoonekana mara chache tu) na galaksi ya Andromeda (inayoonekana kama nyota 1) nyota zote ni majua kama jua letu. Si rahisi kuona nyota nyingi tukiwa mjini penye nuru nyingi wakati wa usiku kwa sababu mwanga wa taa za mjini unaakisiwa katika angahewa na kuleta matata ya kuona mwanga kutoka nje ya angahewa.

Nyota zilizo nyingi za Njia Nyeupe hatuwezi kuziona wala kubainisha kwa hiyo zinatokea machoni kama ukungu mweupe tu.

Uwezo wetu kuona nyota nyingi umepungukiwa na kuwepo kwa mavumbi ya kinyota kati ya mahali petu na kitovu cha galaksi.

Muundo

Galaksi yetu ina umbo la parafujo (spirali) ya kisahani. Mahali petu pamoja na jua pako kando kiasi ndani ya uwiano wa kisahani hiki. Tuko takriban 2/3 ya umbali wa kipenyo kutoka kitovu cha kisahani.

Ikitazamiwa kutoka juu galaksi yetu ina umbo la parafujo lenye mikono mbalimbali. Picha hii tumepata kutokana na kuangalia galaksi za mbali angani zinazoonekana kutoka juu na parafujo inaonekana.

Ikitazamiwa kutoka juu galaksi huwa na mikono mbalimbali ya parafujo.

Marejeo

  • yaani njia ya kondoo wa Ismaili; kuhusu majina ya nyota na sayari zilizojulikana kwa Waswahili na hivyo kuwa na majina asilia linganisha Jan Knappert, Swahili Islamic poetry, Brill 1971, Vol 1 uk 96-97 - taz google booksearch [1]
  • Soma pia

    Viungo vya Nje

    Wikimedia Commons ina media kuhusu: