Tofauti kati ya marekesbisho "Periplus ya Bahari ya Eritrea"

Jump to navigation Jump to search
no edit summary
'''Periplus ya [[Bahari ya Eritrea]]''' ni kitabu cha mwongozo kwa ajili ya mabaharia kilichoandikwa mn. mw. 70 b.K.. "Periplus" ni neno la [[Kigiriki]] linalomaanisha tendo la kuzunguka baharini kwa [[merikebu]]; Bahari ya Eritrea ni jina la kale kwa ajili ya [[Bahari ya Shamu]] pamoja na [[Bahari Hindi]]. Jina limeundwa na watu wa nchi za mashariki ya Bahari ya Kati ([[Mediteraneo)]] na [[Misri]] waliotumia lugha ya Kigiriki wakati wa miaka 2000 iliyopita.
 
Kitabu hiki kimeandikwa na mwenyeji wa [[Aleksandria]] / Misri ilikuwa mji mkubwa wakati ule na kitovu cha biashara ya kimataifa kati ya [[Dola la Roma]], [[Afrika ya Mashariki]] na Bara Hindi.
 
Kitabu cha Periplus kinaeleza mabandari kuanzia [[Misri]] hadi [[Afrika ya Mashariki]] kwa upande moja na hadi [[Bara Hindi]] kwa upande mwingine. Kinataja majina ya mabandari, bidhaa zilizopelekwa huko na bidhaa zilizopatikana kila mahali. Pia kuna habari za kando juu ya watu, watawala ni mila zao.
 
Maelezo ni mengi kuhusu pwani la [[Eritrea]] na [[Somalia]] hadi [[Pembe la Afrika]]; kuelekea kusini majina ya mabandari ni machache; mwisho wa eneo lililojulikana ni mji wa [[Rhapta]] katika nchi za [[Azania]].

Urambazaji