Mtakatifu Paulo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: rw:Mutagatifu Pawulo
d roboti Nyongeza: am:ጳውሎስ
Mstari 46: Mstari 46:


[[af:Paulus van Tarsus]]
[[af:Paulus van Tarsus]]
[[am:ጳውሎስ]]
[[an:Sant Pavlo]]
[[an:Sant Pavlo]]
[[ar:بولس الطرسوسي]]
[[ar:بولس الطرسوسي]]

Pitio la 22:07, 24 Januari 2011

Sanamu ya Mtakatifu Paulo mbele ya Kanisa kuu la Roma.

Mtume Paulo ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa.

Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma chini ya Kaisari Nero.

Maisha kabla ya uongofu

Mtakatifu Paulo (7-67 ?) alizaliwa kati ya miaka 7-10 BK katika familia ya Kiyahudi ya kabila la Benyamini (Israeli) na madhehebu ya Mafarisayo iliyoishi katika mji wa Tarsus (kwa sasa mji huo uko sehemu ya kusini mashariki ya nchi ya Uturuki).

Jina lake la kwanza (la Kiebrania) lilikuwa Sauli, lakini kadiri ya desturi ya wakati ule alikuwa pia na jina la Kigiriki: Paulos kutoka Kilatini Paulus (= mdogo). Mwenyewe alikuwa na uraia wa Roma kama wananchi wote wa Tarsus.

Angali kijana alisomea ualimu wa Sheria (yaani wa Torati) huko Yerusalemu chini ya mwalimu maarufu Gamalieli wa madhehebu ya Mafarisayo.

Akishika dini yake kwa msimamo mkali akawa anapinga Ukristo kwa kuwakamata, kuwatesa na hata kuwaua Wakristo, mpaka alipotokewa na Yesu Kristo mfufuka akiwa njiani kwenda Damaski (kwa umuhimu wake katika Historia ya Wokovu habari hii inasimuliwa mara tatu katika kitabu cha Matendo ya Mitume: 9:1-19; 21:12-18 na 22:5-16).

Baada ya uongofu

Baada ya kufanya utume katika mazingira ya Kiarabu, Tarsus na Antiokia alianza kufanya safari za kitume, akienda mbali zaidi na zaidi, akilenga kumhubiri Yesu mahali ambapo bado hajafahamika, hata Hispania.

Muda wote wa utume wake Paulo alipambana na dhuluma kutoka kwa Wayahudi wenzake na matatizo mengine kutoka Wakristo wenye msimamo tofauti na wa kwake hasa kuhusu haja ya kufuata masharti ya Agano la Kale ili kupata wokovu.

Hatimaye alikamatwa na wapinzani wake Wayahudi mjini Yerusalemu, lakini askari wakoloni walizuia asiuawe.

Baada ya hapo alilazimika kukaa gerezani akisubiri hukumu ya Dola la Roma, kwanza Kaisaria Baharini miaka miwili, halafu akakata rufaa kwa Kaisari akapelekwa Roma, alipofika mwaka 61 akakaa miaka miwili tena kifungo cha nje katika nyumba ya kupanga.

Kisha kufunguliwa (labda kwa sababu washtaki wake hawakuwasili) alisafiri tena ingawa hakuna hakika alielekea wapi.

Kifodini chake

Aliuawa nje ya kuta za Roma kwa kukatwa kichwa wakati wa dhuluma za Nero kati ya mwaka 64 na 67 B.K.

Juu ya kaburi lake lilijengwa kanisa kubwa ambalo liliteketea kwa moto katika karne ya 18 likajengwa upya na hadi leo linapokea hija za Wakristo wengi, hasa katika Jubilei ya mtume Paulo iliyotangazwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kwa mwaka 2008/2009.

Maandiko yake

Agano Jipya

Kati ya barua nyingi alizoandikwa kwa makanisa ya Thesalonike, Korintho, Galatia, Roma, Filipi, Kolosai, Efeso, kwa viongozi Wakristo kama Timotheo na Tito, tena kwa Filemoni, katika Agano Jipya zinatunzwa 13.

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtakatifu Paulo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA