Kupanda kwa halijoto duniani : Tofauti kati ya masahihisho
d r2.5.2) (roboti Nyongeza: io:Globala varmesko |
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: als:Globale Erwärmung |
||
Mstari 86: | Mstari 86: | ||
[[af:Aardverwarming]] |
[[af:Aardverwarming]] |
||
[[als:Globale Erwärmung]] |
|||
[[an:Escalfamiento global]] |
[[an:Escalfamiento global]] |
||
[[ang:Ƿoruldlicu ƿearmung]] |
[[ang:Ƿoruldlicu ƿearmung]] |
Pitio la 11:39, 8 Januari 2011
Kupanda kwa halijoto duniani kunaonekana kwa kulinganisha vipimo vya halijoto vinavyopatikana. Kupanda huku kunaleta mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoanza tayari kuathiri maisha ya watu na uhai duniani kwa ujumla.
Kuna hofu ya kwamba mabadiliko haya yataleta hatari kubwa kwa jamii za watu.
Kati ya wanasayansi kuna tofauti ya maoni kama sababu za mabadiliko ni shughuli za kibinadamu au kama kuna sabau asilia. Siku hizi wataalamu wengi wanafikiri ya kwamba sababu kuu ni kuchoma kwa makaa na mafuta katika viwanda, magari na vituo vya umeme kunachopuliza gesi hewani kama dioksidi kabonia.
Vipimo na data
Duniani kuna upimaji wa kisayansi wa halijoto tangu mwaka 1860. Kabla ya hayo kuna kumbukumbu ya hali ya hewa katika karne zilizopita kutoka mahali mbalimbali ambazo hazikusanifishwa wakati ule. Leo hii wanasayansi wanatumia vipimo na taarifa za kale wakipiga makadirio juu ya hali ya hewa katika historia.
Hapo wanatumia pia mbinu kama kulinganisha miviringo kwenye mashina ya miti inayonyesha miaka yenye mvua mwingi au kidogo au wanapima kiwango cha dioksidi kabonia kwenye barafu ya chini nchani yenye umri wa miaka 10,000 na zaidi.
Kwa jumla makadirio ya hali ya hewa hutofautiana lakini kwa jumla kuna picha juu ya miaka 1,000 iliyopita. Watalaamu wanakubaliana ya kwamba mnamo mwaka 1000 kulikuwa na kipindi cha joto kiasi na tena kipindi cha baridi kiasi kuanzia manmo mwaka 1600.
Lakini hakuna uhakika bado juu ya athira duniani kwa sababu sehemu kubwa ya data ni kutoka upande wa kaskazini ya dunia.
Vipimo vya kisayansi vinavyopatikana vinaonyesha ya kwamba halijoto ya wastani duniani imepanda sentigredi 0.7 kati ya 1906 na 2005. Hii si kiwango kidogo; wakati wa zama za barafu kubwa miaka 100,000 iliyopita halijoto ilikuwa tu 6 °C chini ya wastani ya leo na hii ilitosha kufunika seehmu kubwa za Ulaya, Asia na Amerika ya Kaskazini na mabapa manene ya barafu.
Dalili zote zinadokeza ya kwamba kupanda kwa halijoto kuliharakishwa tangu 1970 na kunaelekea kupanda zaidi.
Sababu za kuongezeka kwa halijoto
Kwa miaka kadhaa wataalamu hawakukubaliana juu ya sababu za kongezeka kwa halijoto. Kwa jumla kuna maelezo mawili tofauti:
- Kupanda kwa halijoto ni jambo la kawaida lenye sababu asilia; historia inaonyesha vipindi vya joto na vipindi vya baridi na sababu kuu ni mabadiliko ya kiwango cha mnururisho wa jua uanofika duniani. Mabadiliko haya hayakueleweka bado lakini labda kuna kitu kama majira ya jua yenyewe yanaobadilia kila baada ya miaka mia kadhaa.
- Kupanda wa halijoto kwa sasa si jambo la kawaida kwa sababu kunaenda sambamba na kuongezeka kwa gesi kama dioksidi kabonia hewani kutokana na shughuli za kibinadamu hasa kuchoma kwa makaa na mafuta ya petroli.
Siku hizi wataalamu wengi wanelekea upande wa pili maana wanaona mbali na sababu asilia kuna athira za kibinadamu zinazobadilisha hali ya hewa.
Matokeo yanayotarajiwa
Wataalamu wanaonya ya kwamba kupanda kwa halijoto inaweza kuleta mabadiliko kama yafuatayo:
- kuongezeka kwa halijoto ya angahewa itaongeza pia halijoto ya bahari na kusababisha uvukizaji mkubwa utakaoleta mawingu na mvua wa nyongeza duniani
- mikondo ya bahari itabadilika na kubadilisha hali ya hewa katika nchi nyingi
- sehemu kadhaa penye jangwa zitapokea mvua lakini maeneo mengine yatakosa mvua hivyo kuleta matatizo kwa kilimo na njaa kwa watu
- barafu kwenye ncha za dunia itaendelea kuyeyuka. Hii itasababisha kupanda kwa uwiano wa bahari, kuleta mafuriko kwenye pwani za dunia na kuhatarisha makazi ya watu karibu na bahari hasa miji ya bandari na nchi za visiwani. Nchi kadhaa kama Maldivi zitazama baharini na kupotea kabisa.
- Kwa jumla upepo na tufani zitaongezeka na kuwa kali zaidi
- Magonjwa kama malaria yataongezeka kwa sababu mbu wanaopitisha ugonjwa watapata nafasi mpya katika sehemu zilizokuwa baridi mno hadi sasa
Viungo vya Nje
Vipimo na data
- Global Warming Wikia
- NOAA CMDL CCGG - Interactive Atmospheric Data Visualization NOAA CO2 data
- UNEP - The present carbon cycle - Climate Change carbon levels and flows
- Temperature data Climatic Research Unit, University of East Anglia, Norwich, UK. Philip D. Jones and other.
- Hadley Centre: Global temperature data
Swali la dioksidi kabonia
- International Energy Annual: Reserves
- IEA Publications Bookshop - Key World Energy Statistics
- International Energy Annual 2002: Carbon Dioxide Emissions
Tovuti za kisayansi
- NASA's Global Hydrology and Climate Center
- NASA's Goddard Institute for Space Studies (GISS) — Global Temperature Trends.
- NASA's GISS paleoclimate site
- National Oceanic and Atmospheric Administration — NOAA, United States Department of Commerce — Global Warming FAQ
- NOAA's paleoclimate site
- MIT Joint Program on the Science and Policy of Global Change
- Real climate a blog where scientists discuss the science of global warming
Habari za ziada
- New Scientist: Climate Change — Latest news, articles and FAQ on climate change from New Scientist magazine.
- Discovery of Global Warming — An extensive introduction to the topic and the history of its discovery
- Science of Climate Change — Meteorological Service of Canada, a guide to understanding the science behind climate change with a thorough FAQ section.
- Global warming - a briefing document, summarising current arguments concerning global warming. They present various points of view and some of the basic problems in following the science.
- How To Help Prevent Global Warming Articles And Newsletter
- Karaca, M. Şen, Ö.L. 2007. Küresel Isınma: Gerçekler ve Belirsizlikler, Avrasya Yer Bilimleri Enstitüsü, İstanbul Teknik Üniversitesi
- http://www.sunnyvalecool.org/ We are a team of Sunnyvale, California, residents and friends.
Mengine
- A large compendium of links to sites with information on global warming
- Ross McKitrick's commented list of resources on global warming
- Science and Technology Librarianship: Global Warming and Climate Change Science — Extensive commented list of Internet resources — Science and Technology Sources on the Internet.
- Activist Magazine: Carbon Activism for Beginners
- Stop Climate Chaos ~ ACT for the Earth
Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA