Kanada : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: ang:Cænada
Mstari 286: Mstari 286:
[[roa-rup:Canada]]
[[roa-rup:Canada]]
[[ru:Канада]]
[[ru:Канада]]
[[rw:Kanada]]
[[sa:केनडा]]
[[sa:केनडा]]
[[sah:Канаада]]
[[sah:Канаада]]

Pitio la 09:39, 28 Desemba 2010

Kanada

Kanada ni nchi kubwa ya Amerika ya Kaskazini. Mji mkuu ni Ottawa. Ni nchi kubwa duniani baada ya Urusi lakini idadi wa wakazi ni milioni 32 tu. Kwenye nchi kavu imepakana na Marekani bara na jimbo la Alaska. Mbele ya pwani zake kuna kisiwa kikubwa cha Greenland ambayo ni chini ya Denmark halafu visiwa vidogo vya St. Pierre na Miquelon (Ufaransa).

Jiografia

Kanada ni nchi kubwa ya pili duniani lakini maeneo mengi ni baridi mno hawana watu. Pwani la Kanada ni ndefu kushinda nchi zote za dunia ikipakana na Atlantiki, Pasifiki na Bahari ya Aktika.

Jumla ya wakazi milioni 32 huishi katika majimbo 10 na maeneo matatu ya kitaifa.

Katika eno la 9,984,670 km² ni 9,093,507 km² nchi kavu na 891,163 km² maji. Umbali kutoka Rasi Columbia kwenye kisiwa cha Ellesmere katika kaskazini hadi kisiwa cha kisiwa cha Middle Island katika ziwa la Erie jimboni Ontaria ni 4,634 km.

Umbali kutoka Rasi Spear katika Newfoundland upande wa mashariki hadi mpaka na Alaska upande wa magharibi ni 5,514 km.

Historia

Maneo ya Kanada yalikaliwa tangu miaka 50,000 hadi 15,000 iliyopita na wahamiaji kutoka Asia ya Kaskazini.

Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa Wanorwei kutoka Greenland mnamo mwaka 1000 BK. Lakini hawakukaa muda mrefu sana. Katika karne zilizofuata kuna uwezekano ya kwamba wavuwi kutoka Ulaya ya Kaskazini walifika pwani za Kanada mara kwa mara na kujenga makazi ya muda wakikausha samaki kwa ajili ya sfari za kurudi lakini hakuna uhakika.

26 Aprili 1497 alifika Mwitalia Giovanni Caboto (kwa Kiingereza huitwa "John Cabot") kwenye visiwa vya Newfoundland akiwa katika utumishi wa malkia wa Uingereza akavitangaza kuwa eneo la Kiingereza.

Mnamo 1534/1535 Wafaransa walifika katika eneo la Mto Saint Lorensi na kujenaga makao yao.

Wapelelezi na walowezi kutoka Ulaya walileta nao magonjwa ambayo hayakujulikana kwa wenyeji asilia na kusababisha vifo vingi kati yao. Kupunguzwa kwa wakazi asilia kulisaidia upanuzi wa walowezi Wazungu kota Amerika.

Koloni za Waingereza na Wafaransa zilikua polepole. Katika Vita ya Miaka Saba Ufaransa ilipotea maeneo yake yote yaliyotwaliwa na Uingereza. Visiwa vya St. Pierre na Miquelon pekee vilibaki upande wa Ufaransa. Uingereza iliamua kukubali utamaduni wa pekee wa wakazi Wafaransa katika jimbo la Quebec. Hadi leo wanaendelea kutumia Kifaransa na kufuata hasa Ukatoliki tofauti na Wakanada wenye asili ya Kiingereza walio zaidi Waprotestanti.

Wakati wa vita ya kupigania uhuru wa Marekani wakazi wa Kanada walibaki upande wa Uingereza. Hivyo Kanada iliendelea chini ya Uingereza ikaitwa "Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza".

1841 sehemu mbaimbali ziliunganishwa kama koloni moja ya Kanada. 1867 Bunge la Uingereza lilikubali sheria iliyounda Shirikisho la Kanada lenya majimbo manne ya Ontario, Quebec, Nova Scotia na New Brunswick. Sasa Kanada ilikuwa nchi ya kujitawala chini ya Mfalme wa Uingereza.

Kujengwa kwa reli kati ya Atlantiki na Pasiki na kufika kwa wahamiaji kutoka Ulaya kuliimarisha nchi mpya. Majimbo mapya yaliundwa hadi kufika majimbo 10 na maeneo matatu chini ya shirikisho jinsi ilivyo sasa.

Kanada ilishikamana na Uingereza katika vita kuu za dunia zote mbili. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi ilionekana kama nchi ya pekee iliyotoa sahihi yake pekee na Uingereza chini ya mkataba wa Versailles. 1927 ilimpeleke balozi wa kwanza Marekani. Uhuru kamili ilipatikana 1982. Hadi leo malkia wa Uingereza ni mkuu wa dola akiwakilishwa na gavana mkuu.

Miji

Zaidi ya nusu ya wakazi hushi katika miji mikubwa zaidi. Mji mkubwa ni Toronto yenye wakazi milioni 5.6 ambayo ni bandari kwenye Ziwa Ontario na kitovu cha viwanda. Montreal ni mji wa biashara mwenye milioni 3.27.

Miji mingine mikubwa ni (idadi ya wakazi katika mabano):

Majimbo

Ramani ya Kanada na majimbo yake
  1. Alberta - AB
  2. British Columbia - BC
  3. Manitoba - MB
  4. New Brunswick - NB
  5. Newfoundland and Labrador
  6. Northwest Territories - NT
  7. Nova Scotia - NS
  8. Nunavut - NU
  9. Ontario - ON
  10. Prince Edward Island - RE
  11. Quebec - (Kifaransa) PQ (Kiingereza) QC
  12. Saskatchewan - SK
  13. Yukon - YU

Watu na lugha

Wakazi asilia wa Kanada ni Maindio na Maeskimo. Walikuwa wameingia kutoka Siberia (Asia) Hakuna uhakika walikuwa wangapi wakati wa kufika kwa Wazungu lakini idadi yao ilipungua haraka kwa sababu watu kutoka Ulaya walileta magonjwa ya kuambukizwa na wenyeji walikosa kinga dhidi yao. Leo hii idadi imeongezeka tena kiasi kuna takriban milioni 1.2 au asilimia 4 wa Wakanada wote.

Wahamiaji kutoka Ùfaransa walitangulia wakifuatwa na Waingereza, Waskoti na Waeire. Wengine walifuata kutoka Ujerumani, Italia, Urusi, Ukraine, Poland na penginepo. Katika miaka ya nyuma wahamiaji wengi wamefika kutoka China na Asia. Wahindi wengi waliofukuzwa Uganda wamehamia Kanada pia.#

Lugha rasmi ni Kiingereza na Kifaransa.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA