Kahawa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: wuu:咖啡
Mstari 131: Mstari 131:
[[ro:Cafea]]
[[ro:Cafea]]
[[ru:Кофе]]
[[ru:Кофе]]
[[rw:Ikawa]]
[[sah:Кофе]]
[[sah:Кофе]]
[[scn:Café]]
[[scn:Café]]

Pitio la 22:16, 27 Desemba 2010

Kwa maana mengine ya jina hili angalia Kahawa (maana)

Kikombe cha kahawa

Kahawa ni kinywaji kinachotengezwa kutokana na buni ambazo ni mbegu za mibuni.

Kahawa ni kinywaji kinachozidi kuenea duniani. Inapendwa kwa sababu ya ladha yake pamoja na dawa la kafeini lililopo ndani yake. Kafeini ina taathiri ya kuchechemua na kuondoa uchovu.

Matumizi ya kahawa

Kuchemsha unga wa kahawa pamoja na maji ni njia asilia

Wanywaji wkuu wa kahawa duniani ni watu wa Ufini wanaotumia kilogramu 11.3 kwa mwaka na kila mkazi ambayo ni sawa na vikombe 1737 kwa mwaka au vikombe 5 kwa siku kwa kila mkazi. Lakini watoto hawanywi kahawa hivyo watu wazima hunywa zaidi kuliko wastani hii.

Wakazi wa Marekani lkatika mwaka 1998 walitumia kahawa tani 1.148.000 inayolingana na wastani ya matumizi ya vikombe 1.8 kwa siki na kila mkazi.

Wajerumani huwa na wastani wa vikombe 4 kwa siku hii ni zaidi kuliko matumizi yao ya bia.

Njia za kutengeneza kahawa

Buni zilizokaangwa hupondwa au kusagwa kuwa unga wa kahawa. Mara nyingi kipimo ni kijiko kidogo kimoja cha unga kwa kila kikombe cha kahawa.

Kuna njia mbalimbali za kutengeneza kahawa zinazotofatiana kati ya nchi na nchi. Watu wanakoroga sukari au maziwa katika kahawa kulingana na mapenzi yao.

  • Kahawa ya kuchemsha: unga pamoja na maji hukorogwa katika sufuria juu ya moto na kuchemka polepole. Njia hii hupendwa katika nchi za Mashariki ya Kati, Afrika ya Kaskazini, Uturuki na Ugiriki. Inapatikana pia katika Uswahilini kama desturi yenye asili ya Uarabuni.
  • Espresso: Unga huwekwa katika ya chujio ndani ya mashine na maji ya kuchemka hupitishwa kwa shindikizo katika unga. Asili ya mashine hizi ni Italia lakini zimeenea duniani. Kahawa yake ni nzito lakini inakorogwa mara nyingi pamoja na maziwa au povu ya maziwa.
  • Kahawa ya filta: Umga huwekwa katika mfuko wa karatasi ya filta juu ya birika na maji ya kuchemka humwagwa juu yake yakitirikika chini polepole. Kuna pia filta za metali. Mara nyingi watu wanatumia machine wakijaza unga kwenye filta na maji kwenye chobo cha mashina na kuwasha macine tu inayochemsha maji yanayotiririka polepole kuingia katika filta.
  • Kuna pia birika au machine zinazoiga mwendo wa esperesso lakini bila shindikizo kali hivi. Kwa mfano kuna birika ambako unga na maji ya kuchemka zinamwagiliwa pamoja. Mchanganyiko unakaa kwa dakika moja mbili, halafu kuna chujio kwneye mfuniko wa birika inayosukumwa chini polepole. Unga unashikwa chini na kahawa inapita kukaa juu.
  • kahawa mumunyifu: inatengenezwa kwa kutumia unga wa pekee ulioandaliwa kiwandani. Hapa kahawa inatengenezwa kiwandani halafu maji huondolewa kwenye kahawa na unga unabaki unaokorogwa tu katika maji ya moto na kahawa ni tayari. Watu wengi wameizoea kwa sababu inatengenezwa haraka lakini wapenzi wa kahawa mara nyingi wanalalamika ya kwamba sehemu ya ladha inapotea.


Viungo vya Nje

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA