Wasuni : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: hy:Սուննի իսլամ
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:Islam by country.svg|thumbnail|300px|Nchi za Waislamu wengi na madhehebu<br />Kibichi: Wasunni wengi; Nyekundu: Washia wengi]]
[[Picha:Islam by country.png|thumbnail|300px|Nchi za Waislamu wengi na madhehebu<br />Kibichi: Wasunni wengi; Nyekundu: Washia wengi]]
'''Wasunni''' ni [[dhehebu]] kubwa ndani ya dini ya [[Uislamu]]. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasunni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati ya [[Washia]].
'''Wasunni''' ni [[dhehebu]] kubwa ndani ya dini ya [[Uislamu]]. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasunni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati ya [[Washia]].



Pitio la 17:36, 13 Desemba 2010

Nchi za Waislamu wengi na madhehebu
Kibichi: Wasunni wengi; Nyekundu: Washia wengi

Wasunni ni dhehebu kubwa ndani ya dini ya Uislamu. Takriban asilimia 80 - 90 za Waislamu wote duniani hukadiriwa kuwa Wasunni na wengine 10-20 % huhesabiwa kati ya Washia.

Wasunni huitwa kwa Kiarabu ahl ul-sunna (Kiarabu: أهل السنة; "watu wa mapokeo"). Neno Sunni hutokea kutoka kwa neno sunna (Kiarabu : سنة ) inayomaanisha mapokeo ya Mtume Muhammad.

Isipokuwa Uajemi, Iraki, Bahrain, Azebaijan, Yemen, Omani na Lebanoni kundi kundi kubwa katika nchi zote penye Waislamu wengi.

Historia

Wasunni hufuata mwelekeo wa Uislamu ulioanzishwa na ukhalifa wa Abu Bakr na kutokubali uongozi wa familia ya Mtume Muhammad kupitia Ali, Hassan na Husain.

Madhehebu ya Wasunni

Kati ya Wasunni kuna madhehebu nne zinazotofautiana kiasi kuhusu mafundisho ya sharia au sheria ya kidini ya Kiislamu. Ndio Wahanafi, Wamaliki, Washafii na Wahanbali. Kwa jumla Wasunni hukubaliana ya kwamba madhehebu haya yote manne ni sawa.

Walimu wengine hasa katika kikundi cha Wawahabi kilichoanzishwa kati ya Wahanbali kimekaza mafundisho yake hadi kuwashtaki wengine kuwa si Waislamu wa kweli.


Viungo vya Nje