Urithi wa Dunia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: az:Dünya irsi
Mstari 76: Mstari 76:
[[lv:UNESCO Pasaules mantojuma objekts]]
[[lv:UNESCO Pasaules mantojuma objekts]]
[[mk:Список на светско културно и природно наследство на УНЕСКО]]
[[mk:Список на светско културно и природно наследство на УНЕСКО]]
[[ml:ലോകപൈതൃകസ്ഥാനം]]
[[mn:Дэлхийн өв]]
[[mn:Дэлхийн өв]]
[[mr:जागतिक वारसा स्थान]]
[[mr:जागतिक वारसा स्थान]]

Pitio la 13:00, 11 Novemba 2010

Urithi wa Dunia ni maeneo yenye thamani kubwa ya kiutamaduni au kimazingira duniani yanayoangaliwa na shirika la UNESCO.

Mwanzo wa mwaka 2009 sehemu 878 katika nchi 145 zimekubaliwa. Nchi inayoongoza kwa wingi wa mahali ni Italia yenye 43.

Orodha rasmi ya UNESCO ina mahali 679 pa urithi wa dunia wa kiutamaduni na mahali 174 pa urithi wa dunia wa kimazingira, mbali ya 25 pa mseto.

Mwanzo wa jitihada za kuhifadhi urithi wa dunia ulikuwa ujenzi wa bwawa la Assuan lililoelekea kuzamisha majengo mbalimbali ya utamaduni wa Misri na Nubia wa kale chini ya maji. Wakati ule UNESCO ilifaulu kukusanya pesa ili hekalu la Abu Simbel liweze kuhamishwa mlimani kabla ya kujaa kwa bwawa.

Tangu 1972 kuna mkataba wa kimataifa wa Stockholm kuhusu hifadhi ya urithi wa dunia kiutamaduni na kimazingira. Kila mahali panapopendekezwa ili pakubaliwe panahitaji angalau sifa moja kati ya sita zifuatazo:

  • kuwa na thamani ya pekee ya kisanii
  • kuwa na athira muhimu katika eneo fulani au kipindi cha historia
  • kuwa kitu cha pekee kisichopatikana tena au kuwa na umri mkubwa
  • kuwa mfano bora wa kipindi fulani cha historia ya ujenzi
  • kuwa muhimu katika uhusiano na fikra muhimu au watu muhimu wa historia

Kamati ya World Heritage Committee hukutana kila mwaka na kuangalia maombi ya kupokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Kamati inapokea taarifa kuhusu hifadhi na hali ya urithi uliopo tayari orodhani. Kila baada ya miaka miwili orodha inatolewa upya.

Viungo vya nje

Kigezo:Link FA