Wapangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: en:Pangwa people
d →‎Viungo vya Nje: ainisha {{mbegu}} using AWB
Mstari 16: Mstari 16:
[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]
[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]


{{mbegu}}
{{mbegu-utamaduni-TZ}}
{{DEFAULTSORT:Pangwa}}
[[Category:Makabila ya Tanzania|P]]

[[Jamii:Makabila ya Tanzania]]


[[en:Pangwa people]]
[[en:Pangwa people]]

Pitio la 13:18, 4 Novemba 2010

Wapangwa ni kabila kutoka Milima Livingstone karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa Nyasa, wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Iringa, kusini ya nchi ya Tanzania. Mwaka 2002 idadi ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 95,000.

Chakula chao ni ugali wa mahindi, ulezi na mtama kidogo. Kitoweo cha vyakula hivyo ni maharage, samaki, nyama na jamii ya mboga mboga. Kinywaji chao ni pombe (ukhimbi) yaani kangala, komoni, ulanzi ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi.

Hulima mazao mbalimbali katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito. Ni wafugaji wa ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe (kitimoto). Pia hulima mazao ya biashara kama kahawa, chai, pareto, mahindi. Kabila hili pia hupata matunda ya asili kama vile; masada, savula, makuhu, mahofita, minhingi, vudong'o na nisongwa.

Usafiri wao wa maji ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.

Nyumba zao za asili kwa sasa ni za matofali ya udongo ya kuchoma na kuezekwa kwa bati, hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti asili kugandikwa kwa udongo wa mfinyanzi na kuezekwa kwa nyasi aina ya hunji na lihanu.

Mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa,hufumwa na kupakwa mono.

Lugha yao ni Kipangwa.

Viungo vya Nje

Ethnologue

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wapangwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.