Jakaya Kikwete : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: cs:Jakaya Kikwete
d roboti Nyongeza: pt:Jakaya Kikwete
Mstari 59: Mstari 59:
[[no:Jakaya Kikwete]]
[[no:Jakaya Kikwete]]
[[pl:Jakaya Kikwete]]
[[pl:Jakaya Kikwete]]
[[pt:Jakaya Kikwete]]
[[ro:Jakaya Mrisho Kikwete]]
[[ro:Jakaya Mrisho Kikwete]]
[[ru:Киквете, Джакайя]]
[[ru:Киквете, Джакайя]]

Pitio la 00:41, 29 Oktoba 2010

Jakaya Mrisho Kikwete tangu tarehe 21 Desemba 2005 ni rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jakaya Kikwete pamoja na marais waliostaafu Benjamin Mkapa na Alhaji Ali Hassan Mwinyi

Asili

Amezaliwa 7 Oktoba, 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani. Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.

Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga. Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, Babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.

Masomo

1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Middle School Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga. Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza digrii yake mwaka 1978. Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.

Kupanda ngazi katika siasa

1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mw. 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.

1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwl. Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia Benjamin Mkapa nafasi aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri ya Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.

Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.


Viungo vya nje