Teresa wa Mtoto Yesu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 104: Mstari 104:
[[fr:Thérèse de Lisieux]]
[[fr:Thérèse de Lisieux]]
[[ga:Naomh Thérèse de Lisieux]]
[[ga:Naomh Thérèse de Lisieux]]
[[gd:Naomh Thérèse de Lisieux]]
[[hr:Sveta Mala Terezija]]
[[hr:Sveta Mala Terezija]]
[[hu:Lisieux-i Szent Teréz]]
[[hu:Lisieux-i Szent Teréz]]

Pitio la 03:12, 1 Oktoba 2010

Faili:TeresadiLisieux.JPG
Picha ya Teresa akiwa amevaa kanzu na shela za Kikarmeli, 1895.

Teresa wa Mtoto Yesu na wa Uso Mtakatifu ni jina la kitawa la Thérèse Françoise Marie Martin, maarufu pia kwa jina la Teresa wa Lisieux, anayeheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu mwenye sifa za bikira na mwalimu wa Kanisa.

Tangu mwaka 1927 ni msimamizi wa wamisionari wote (pamoja na Fransisko Xavier), na tangu mwaka 1944 wa Ufaransa (pamoja na Yoana wa Arc).

Alizaliwa Alençon tarehe 2 Januari 1873. Wazazi wake walikuwa Louis Martin na Marie-Azélie Guérin, ambao wanaheshimiwa kama wenye heri.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Oktoba.

Maisha

Teresa mwaka 1881 akiwa na umri wa miaka 8.
Teresa muda mfupi kabla ya kusafiri kwenda Italia (1887)
Faili:Teresadarco.jpg
Teresa akiigiza kama Yoana wa Arc (1895)
Basilika la Lisieux, lenye eneo la 4500 m2 na urefu wa mita 95, lililojengwa kwa heshima yake mwaka 1937

Teresa, mtoto wa tisa na wa mwisho wa Louis Martin na Marie-Azélie Guérin (Zélie), alizaliwa tarehe 2 Januari 1873 kwenye barabara rue Saint-Blaise 42, huko Alençon (Ufaransa).

Walipokuwa vijana wazazi wake walitaka kuingia utawani, wasiweze. Baada ya kuoana, maisha yao yote yaliongozwa na imani na maadili ya Ukristo.

Teresa alipozaliwa, watoto 4 walikuwa wameshafariki.

Teresa alifiwa mama yake alipokuwa na umri wa miaka 4 tu. Hapo mjomba wake, Isidore Guerin, aliteuliwa kuwa mlezi msaidizi wa mabinti watano wa marehemu. Hivyo, tarehe 15 Novemba 1877, Louis Martin alihamia Buissonnets, kitongoji cha Lisieux, awe jirani na shemeji yake mwenye famasia. Huko alijenga uhusiano mkubwa na binamu yake Maria.

Uhusiano wa pekee hasa alikuwa nao kwa dada zake Paulina na Maria, akiwaona kama mama zake.

Mwaka 1882, Paulina alipoingia monasteri ya Wakarmeli ya Lisieux, angetaka kumfuata, lakini hakuweza kutokana na umri wake mdogo. Zaidi tena alitaka kufanya hivyo Maria pia alipoingia monasteri hiyo mwaka 1886.

Usiku wa Noeli iliyofuata, alishinda moja kwa moja huzuni yake iliyomfanya alielie daima. Alielewa anahitaji kumtafuta Mungu zaidi na kujipatia hivyo "Elimu ya upendo.

Alipofikia umri wa miaka 14 Teresa alianza kupigania wito wake dhidi ya upinzani wa watu mbalimbali waliotaka kuahirisha hatua ya kujiunga na utawa. Kwa ajili hiyo alisafiri hadi Roma ili akaombe ruhusa ya Papa Leo XIII, lakini alikataliwa kwa wema, kitu kilichomsikitisha lakini bila ya kumhangaisha, akijua amefanya kila aliloweza ili kuitikia wito wake mapema.

Wakati wa kurudi Ufaransa, askofu wake aliamua kubadili msimamo wake na kumruhusu. Hivyo tarehe 9 Aprili 1888 msichana Teresa alingiia Karmeli, akiwa na miaka 15 tu.

Mwaka 1893 aliteuliwa kuwa mlezi msaidizi wa wanovisi, kazi aliyofanya kwa bidii na ufanisi mkubwa.

Mwaka 1894, baada ya ugonjwa wa muda mrefu, mzee Louis Martin alifariki, na binti yake mwingine, Selina, aliyekuwa anamtunza, aliweza kujiunga na monasteri hiyo. Kamera yake imetuachia picha halisi za Teresa.

Mwezi Aprili 1896, alipatwa na TB, ugonjwa ambao ukaja kumuua baada ya miezi 18. Mateso ya mwili yaliendana na yale ya ndani yanayojulikana kama "usiku wa roho".

Tarehe 10 Julai 1897 udhaifu ulimzuia asiendelee kuandika habari za maisha yake kama alivyoagizwa. Neno la mwisho aliloliandika katika sentensi isiyomalizika ni "upendo".

Alifariki tarehe 30 Septemba, mnamo saa 19:20.

Heshima baada ya kufa

Mara baada ya kufa maandishi yake yalianza kusambaa kwa namna ya ajabu na kumvutia heshima ya wengi. Pia ilipatikana miujiza iliyopatikana kwa maombezi yake.

Mwaka 1925 Papa Pius XI alimtangaza mtakatifu, na mwaka 1997 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwalimu wa Kanisa kutokana na mchango wake mkubwa katika teolojia ya Kiroho alioutoa kupitia maandishi yake, yaliyoenea upesi ajabu duniani kote.

Tafsiri ya Kiswahili na ya Kihaya

THERESIA WA MTOTO YESU, Ua la Upendo, Maisha ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu Aliyoyaandika Yeye Mwenyewe – tafsiri ya J. J. Rwechungura – ed. Paulines Publications Africa – Nairobi 1992 – ISBN 9966-21-021-0 THEREZA OW’OMWANA YEZU – Akamuli k’engonzi, Oburora bw’Omutakatifu Thereza Ow’omwana Yezu Obwo Yayehandikire Wenene – tafsiri ya J. J. Rwechungura – ed. Marianum Press Kisubi – Kisubi 1960

Viungo vya nje

Filamu juu yake

Picha zake

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

Kigezo:Link FA