Mita : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: io:Metro
d roboti Badiliko: pt:Metro (unidade de medida)
Mstari 213: Mstari 213:
[[pms:Méter]]
[[pms:Méter]]
[[pnb:میٹر]]
[[pnb:میٹر]]
[[pt:Metro]]
[[pt:Metro (unidade de medida)]]
[[qu:Mitru]]
[[qu:Mitru]]
[[ro:Metru]]
[[ro:Metru]]

Pitio la 17:44, 27 Septemba 2010

Mita ni kipimo cha urefu kimekuwa kipimo sanifu cha kimataifa. Neno limetokana na Kigiriki μέτρον/métron = kipimo, pia chombo cha kupimia.

Kutokana na maana hiyo "mita" inataja pia mitambo ya kupima maji, umeme na kadhalika. Hapo matumizi ya Kiswahili kinafanana na Kiingereza "meter".

Mita ya kimataifa, Reli ya metali ya platini iliyokuwa mfano halisi wa mita hadi 1960. (NIST)

Mita ya asili

Mita imeundwa kama kipimo wakati wa mapinduzi ya Kifaransa mwaka 1793. Nia ilikuwa kumaliza vipimo vya kale kutokana na viungo vya mwili kama hatua, mkono, mguu na kadhalika. Vipimo hivi asilia vilitofautiana kila mahali; Ujerumani ilikuwa na na futi zaidi ya kumi katika mikoa na majimbo mbalimbali. "Mita" imeamuliwa ni sehemu moja kati ya sehemu milioni 40 za meridiani ya Paris (mstari kutoka ikweta hadi ncha ya kaskazini unaopita mji wa Paris).

Mita ya asili ilichongwa kama reli ya shaba baadaye ya platini ambayo ni metali ngumu sana.

Nchi zote duniani hutumia vipimo vya mita hata kama nchi mbalimbali bado hutumia vipimo vya asilia kufuatana na utamaduni wao. Kwa mfano nchi za mapokeo ya Kiingereza hupenda inchi na futi. Matumizi ya vipimo ya kale katika maisha ya kila siku si kizuizi kupeleka watu angani. Warusi bado wanapenda kipimo cha "verst" (mita 1066,8), Waamerika huhesabu "yard" (mita 0,9144) lakini wote walifaulu kurusha makombora angani - isipokuwa kwa kutumia vipimo vya mita.

Elezo ya mita leo

Tangu 1960 mita imepataniwa ni umbali wa njia inayotembelewa na nuru katika anga pasipo na hewa katika muda wa sekonde 1/299,792,458.


Sehemu ndogo na wingi za mita

Kiasi Jina Kifupi Kiasi Jina Kifupi
100 mita m      
10–1 desimita dm 101 dekamita dam
10–2 sentimita cm 102 hektomita hm
10–3 millimita mm 103 kilomita km
10–6 mikromita µm 106 megamita Mm
10–9 nanomita nm 109 gigamita Gm
10–12 pikomita pm 1012 teramita Tm
10–15 femtomita fm 1015 petamita Pm
10–18 attomita am 1018 examita Em
10–21 zeptomita zm 1021 zettamita Zm
10–24 yoktomita ym 1024 yottamita Ym

Vipimo vya kawaida:

Kilomita (km) : Kilomita moja ni mita 1000

Sentimita (cm): Sentimita ni sehemu ya mia ya mita; mita ina sentimita 100.

Millimita (mm): Millimita ni sehemu ya kumi ya sentimita moja; sentimita ina millimita kumi, mita ina millimita elfu moja.