Wafransisko : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: ro:Ordinele franciscane
Mstari 50: Mstari 50:
[[pl:Zakon Braci Mniejszych]]
[[pl:Zakon Braci Mniejszych]]
[[pt:Ordem dos Frades Menores]]
[[pt:Ordem dos Frades Menores]]
[[ro:Ordinele franciscane]]
[[ru:Францисканцы]]
[[ru:Францисканцы]]
[[sh:Franjevci]]
[[sh:Franjevci]]

Pitio la 23:49, 23 Septemba 2010

Wafransisko ni jina la jumla la wafuasi wote wa Fransisko wa Asizi wanaokadiriwa kuwa milioni moja hivi duniani kote.

Mwanzilishi mwenyewe katika karne XIII alivuta umati wa waamini wa Ukristo katika njia ya toba. Wanaume wengi walimfuata utawani kama Ndugu Wadogo, wanawake walikusanyika monasterini kama Mabibi Fukara Waklara, wengine tena wa jinsia zote mbili walishika Injili katika maisha ya ndoa, upwekeni au kwa kuunda jumuia zisizo na nadhiri.

Matawi hayo yakaja kuitwa Utawa wa Kwanza, wa Pili na wa Tatu. Mapema zilitokea tofauti za mitazamo kuhusu karama halisi ya Mt. Fransisko, hivyo matawi yalianza kugawanyika.

Siku hizi kuna mashirika ya kitawa mia nne hivi yanayofuata mojawapo ya kanuni zilizokubaliwa na mapapa kwa matawi hayo.

Katika ngazi ya kimataifa, Wafransisko wa Kanisa Katoliki wana Baraza la Familia ya Kifransisko ambalo lina uwakilishi katika Umoja wa Mataifa kama Asasi Isiyo ya Kiserikali kuu kuliko zote.

Kuna wafuasi wa Mt. Fransisko hata katika madhehebu mengine, na hasa Waanglikana ambao wana mashirika ya kitawa ya Kifransisko.