Sifuri halisi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 21: Mstari 21:
[[af:Absolute nul]]
[[af:Absolute nul]]
[[ar:صفر مطلق]]
[[ar:صفر مطلق]]
[[be:Абсалютны нуль тэмпературы]]
[[bg:Абсолютна нула]]
[[bg:Абсолютна нула]]
[[br:Zero klok]]
[[br:Zero klok]]

Pitio la 12:54, 11 Septemba 2010

Mfano wa mwendo wa atomi ndani ya molekuli ya proteini yani ndani ya mango. Wakati nishati mwendo inaongezeka kila atomi inachezacheza zaidi. Inaonekana jinsi gani molekuli kwa jumla inahitaji nafasi kubwa zaidi kadiri mwendo unavyoongezeka. Hapa ni sababu ya kwamba magimba yanapanuka kiasi yakipashwa moto na kujikaza wakati wa kupoa.
Mfano wa mwendo wa atomi ndani ya gesi (kama hewani). Mkasi wa mwendo unategemea nishati mwendo wa atomi hizi; katika hewa joto zina mbio mkubwa na katika hewa baridi zina mwendo wa polepole zaidi hadi kufikia kiwango cha sifuri halisi ambako zinakaa kimya bila mwendo.


Sifuri halisi kazika fizikia ni kiwango cha halijoto ya duni kabisa inayowezekana.

Ni sawa na vizio −273.15° kwenye skeli ya selsiasi au vizio 0° kwenye skeli ya kelvini.

Kwenye kiwango cha sifuri halisi hakuna mwendo wa mada au molekuli tena. Sababu yake ni ya kwamba halijoto yenyewe kifizikia ni uso mwingine wa mwendo wa mada yaani mwendo wa molekuli na atomi.

Katika hali ya kawaida molekuli za hewa au za kiowevu huwa na mwendo; pia molekuli za gimba mango huwa na mwendo fulani kama kitisiko. Kama mwendo = halijoto inaongezeka tunaona badiliko la gimba mango kuwa kiowevu au gesi. Kinyume chake tunaona jinsi gani maji "baridi" huwa barafu imara maana yake mwendo wa molekuli za H20 imepungua . Pasipo na mwendo tena hakuna joto wala halijoto na hali hii huitwa "sifuri halisi".

Hali hii inasababisha kutokea kwa mambo yasiyo kawaida. Kwa mfano uwezo wa metali wa kupitisha umeme unaongezeka sana kadiri jinsi metali inavyokaribia sifuri halisi.

Hali halisi haiwezekani kukuta mada kwenye hali ya sifuri halisi kabisa lakini katika maabara imewezekana kuikaribia sana.