Babeli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: lv:Babilona
d roboti Nyongeza: is:Babýlon
Mstari 53: Mstari 53:
[[hy:Բաբելոն]]
[[hy:Բաբելոն]]
[[io:Babilono]]
[[io:Babilono]]
[[is:Babýlon]]
[[it:Babilonia]]
[[it:Babilonia]]
[[ja:バビロン]]
[[ja:バビロン]]

Pitio la 18:27, 8 Septemba 2010

Sehemu ya geti ya Ishtar ya Babeli

Babeli ilikuwa mji wa nyakati za kale katika Mesopotamia. Maghofu yake hupatikana karibu na mji wa kisasa wa Al Hillah (Irak) kando ya mto Frati 90 km kusini mwa Baghdad. Babeli ilikuwa mji muhimu wa Mesopotamia kwa karne nyingi na mji mkuu wa milki iliyotawala maeneo makubwa ya Mashariki ya Kati. Inatajwa mara nyingi katika Biblia.

Orodha ya wafalme wake ilianza mnamo mwaka 2300 KK. Mfalme mashuhuri wa kwanza alikuwa Hammurabi.

Babeli ilikuwa mji mkuu wa madola mawili makubwa kabla na baada ya kipindi cha enzi ya Ashuri. Kati ya 1770 KK hadi 1670 KK na mara ya pili kati ya 612 KK na 320 KK inaaminiwa ilikuwa mji mkubwa duniani.

Wakati wa Dola la Pili la Babeli mfalme Nebukadreza II alitawala nchi zote kati ya Palestina (Kanaani) hadi Ghuba ya Uajemi. Bustani ya malkia Semiramis ilikuwa moja ya maajabu saba ya dunia. Piramidi au zigurat kubwa za mji zilikuwa maarufu na mfano wao ni mnara wa Babeli unaotajwa katika Biblia.

Wakati ule jeshi la Babeli liliteka mji wa Yerusalem mwaka 587 KK, kubomoa hekalu ya Suleimani na kuwapeleka Wayahudi hadi Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli. Inaaminika ya kwamba sehemu kubwa za Biblia ya Kiebrania ziliandikwa uhamishoni kule Babeli.

Mwaka 539 KK Wajemia walivamia Dola la Babeli na kuliteka. Babeli iliendelea kuwa mji muhimu katika Dola la Uajemi. Baada ya ushindi wa Aleksander Mkuu juu ya mfalme Mwajemi Darius III ilikuwa chini ya utawala wa Wagiriki. Aleksander alikufa Babeli mwaka 323 KK katika jumba la kifalme la Nebukadreza.

Mwaka 275 KK Wagiriki walijenga mji mkuu mpya wakawalazimisha wakazi wa Babeli kuhamia huko Seleukia. Hii ilikuwa mwisho wa mji ule mkubwa.

Mataifa ya Kale walikumbuka mji wa Babeli kwa muda mrefu. Kitabu cha Ufunuo wa Yohane katika Agano Jipya kilichoandikwa mnamo mwaka 90 BK kinatumia jina la Babeli kama jina la kitendawili kuashiria Roma.