Fransisko wa Paola : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: nah:Francesco di Paola
Mstari 40: Mstari 40:
[[it:Francesco di Paola]]
[[it:Francesco di Paola]]
[[la:Franciscus de Paula]]
[[la:Franciscus de Paula]]
[[nah:Francesco di Paola]]
[[nap:San Franciscu i Paula]]
[[nap:San Franciscu i Paula]]
[[nl:Franciscus van Paola]]
[[nl:Franciscus van Paola]]

Pitio la 05:43, 1 Agosti 2010

Mtakatifu Fransisko wa Paola (kwa Kiitalia Francesco di Paola; 27 Machi, 14162 Aprili, 1507) alikuwa mtawa nchini Italia.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini Papa Leo X kuwa mtakatifu kuanzia mwaka wa 1519. Tarehe ya kifo chake, yaani 2 Aprili pia ni sikukuu yake.

Maisha

Fransisko alizaliwa kwa muujiza katika mji wa Paola, mkoa wa Calabria, Italia, mwaka 1416. Wazazi wake walikuwa wamefikia uzee bila ya kuweza kuzaa, lakini walimuomba Fransisko wa Asizi na kuweka nadhiri kuwa mtoto wao ataitwa Fransisko. Ndipo walipojaliwa kuzaa.

Tangu utotoni alishika maisha magumu ya sala na toba upwekeni.

Alianzisha shirika la watawa wakaa-pweke, ambalo baadaye likawa Utawa wa Wadogo Kabisa, likapata kibali kutoka kwa Papa mwaka 1506. Pamoja na kuahidi mashauri ya Kiinjili matatu ya kawaida, wanaahidi pia kuishi daima kama wakati wa Kwaresima.

Kanuni yake ni ya pekee, ingawa inafuata ile ya Ndugu Wadogo ikiiongezea malipizi makali ya mababu wa jangwani.

Kauli-mbiu yake ilikuwa neno "caritas" (kwa Kilatini, "upendo").

Fransisko alikufa mwaka 1507 huko Tours, Ufaransa alipokuwa ametumwa na Papa.

Tazama pia

Marejeo

  • "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1328


Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.