Shirikisho la Afrika ya Kati : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 20: Mstari 20:
[[bg:Родезия и Нясаленд]]
[[bg:Родезия и Нясаленд]]
[[ca:Rhodèsia i Niassalàndia]]
[[ca:Rhodèsia i Niassalàndia]]
[[da:Føderationen af Rhodesia og Nyasaland]]
[[de:Föderation von Rhodesien und Njassaland]]
[[de:Föderation von Rhodesien und Njassaland]]
[[en:Federation of Rhodesia and Nyasaland]]
[[en:Federation of Rhodesia and Nyasaland]]

Pitio la 18:34, 30 Julai 2010

Bendera ya Shirikisho la Afrika ya Kati
Eneo la Shirikisho la Afrika ya Kati

Shirikisho la Afrika ya Kati iliitwa pia Shirikisho la Rhodesia na Unyasa ikawa dola la kujitawala chini katika mfumo wa ukoloni wa Uingereza uliounganisha nchi za leo za Zambia, Zimbabwe na Malawi zilizoitwa wakati ule Rhodesia ya Kaskazini, Rhodesia ya Kusini na Unyasa (Nyassaland). Ilipatikana kati ya 1953 hadi mwisho wa 1963.

Shirikisho lilianzishwa 1. 08. 1953 kwa shabaha ya kuunda nchi itakayofuata njia kati ya muundo wa ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini upande mmoja na nchi huru zilizotawaliwa na wanasiasa Waafrika wenye mwelekeo wa Ujamaa. Ilikuwa jaribio la kutunza kipaumbele wa walowezi wa asili ya Ulaya.

Mwisho ulikaribia baada ya miendo ya kumaliza ukoloni duniani kote na nguvu ya wawakilishi wa Waafrika katika eneo la shirikisho iliongezeka nguvu. Mwisho wa 1963 Rhodesia ya Kaskazini ilikuwa taifa jipya la Zambia na Uyasa (Nyassaland) ikawa Malawi. Rhodesia ya Kaskazini ilibaki peke yake ikitangaza uhuru wake miaka kadhaa baadaye na baada ya vita ya ukombozi kuwa nchi ya Zimbabwe.