Juma : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: ckb:ھەفتە
d roboti Nyongeza: pnb:اٹھوارہ Badiliko: so:Todobaad
Mstari 129: Mstari 129:
[[pl:Tydzień]]
[[pl:Tydzień]]
[[pms:Sman-a]]
[[pms:Sman-a]]
[[pnb:اٹھوارہ]]
[[pt:Semana]]
[[pt:Semana]]
[[qu:Simana]]
[[qu:Simana]]
Mstari 140: Mstari 141:
[[sk:Týždeň]]
[[sk:Týždeň]]
[[sl:Teden]]
[[sl:Teden]]
[[so:Usbuuc]]
[[so:Todobaad]]
[[sr:Седмица]]
[[sr:Седмица]]
[[stq:Wiek]]
[[stq:Wiek]]

Pitio la 05:09, 11 Juni 2010

Juma au wiki ni kipindi cha siku saba. Kila siku ina jina lake.

Katika mwaka wa kalenda ya Gregori mna majuma 52 pamoja na siku moja au mbili za ziada. Hesabu ya majuma inaendelea mfululizo bila ya kuanza upya wakati wa mwaka mpya. Ufuatano wa juma haulingani na mgawanyo mwingine wa wakati kwa njia ya miezi au mwaka.

Mapokeo ya Kiyahudi-Kikristo

Asili ya juma ni katika utamaduni wa kale wa Mashariki ya Kati tangu Babiloni. Imeenea duniani kote kupitia Biblia na desturi za Uyahudi na Ukristo.

Ufuatano wa siku katika mapokeo haya huanza na Jumapili. Majina ya siku ni kama yafuatayo:

Katika mwaka juma moja la Machi mwishoni au Aprili linaadhimishwa na Wakristo wengi kama Juma kuu, ambapo wanaadhimisha matukio makuu ya imani yao kadiri ya historia ya wokovu, yaani mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.

Siku za Jumamosi na Jumapili mara nyingi huitwa "wikendi" (kutoka Kiingereza: "weekend", yaani mwisho wa juma). Hata hivyo katika mapokeo hayo Jumapili ni mwanzo wa wiki mpya.

Majina ya siku kwa Kiswahili

Majina ya siku tano kwa Kiswahili ni ya namba zinazoanza kuhesabiwa baada ya siku ya Ijumaa (ambayo ni siku ya sala kuu katika Uislamu):

Ijumaa - Jumamosi - Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano.

Alhamisi na Ijumaa ni majina ya lugha ya Kiarabu inayofuata mapokeo ya Kiyahudi kuhusu majina ya siku.

Hivyo "Alhamisi" ina maana ya "siku ya tano" (baada ya Jumamosi inayoitwa "sabat" kwa Kiarabu sawa kama "shabbat" (=sabato) kwa Kiebrania (lugha ya Wayahudi).

"Ijumaa" ni matamshi ya Kiswahili ya jina la Kiarabu la "jum'a" inayomaanisha "siku ya mkutano" (= ya kusali pamoja).

Siku za juma (wiki)
Jumapili - Jumatatu - Jumanne - Jumatano - Alhamisi - Ijumaa - Jumamosi

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA