Chama cha kisiasa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: arz:حزب
Mstari 14: Mstari 14:
[[an:Partito politico]]
[[an:Partito politico]]
[[ar:حزب سياسي]]
[[ar:حزب سياسي]]
[[arz:حزب]]
[[ast:Partíu políticu]]
[[ast:Partíu políticu]]
[[bar:Politische Partei]]
[[bar:Politische Partei]]

Pitio la 09:25, 8 Juni 2010

Chama cha kisiasa ni maungano ya watu wanaotafuta mamlaka katika dola na hasa serikali kwa kusudi la kutekeleza shabaha za kisiasa au kifalsafa pamoja na faida kwa ajili vikundi fulani faida zao za binafsi.

Vyama mara nyingi hutamka mwelekeo au itikadi fulani inayoandikwa katika programu yao.

Katika mfumo wa vyama vingi kila chama kinagombea nafasi za bunge au serikali dhidi ya vyama vingine. Wakati wa uchaguzi kila chama kinapaswa kujieleza, kutetea matendo yake ya nyuma na kuonyesha jinsi gani kinavyotaka kuboresha mambo tofauti na vyama vingine. Kwa njia hii kila chama huchangia kwenye harakati ya kujenga nia ya jamii inamofanya kazi kama inashinda au kushindwa kwenye uchaguzi.

Penye mfumo wa chama kimoja kazi ya chama kitakuwa tofauti. Historia inna mifano ya kwamba chama cha pekee kinaelekea kwenye udikteta kwa viwango tofauti.

Vyama hutofautiana sana kuhusu kiasi cha tofauti za maoni zinazoruhusiwa ndani yao, uhusiano kati ya viongozi na wanachama, kiasi cha uwezo wa wanachama kuathiri mwelekeo wa chama na umuhimu wa programu.