Mwanaanga : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: tr:Uzay insanı
d roboti Nyongeza: sah:Космонаавт
Mstari 77: Mstari 77:
[[ro:Astronaut]]
[[ro:Astronaut]]
[[ru:Космонавт]]
[[ru:Космонавт]]
[[sah:Космонаавт]]
[[scn:Astrunàuta]]
[[scn:Astrunàuta]]
[[simple:Astronaut]]
[[simple:Astronaut]]

Pitio la 09:40, 12 Aprili 2010

Mwanaanga ni mtu anayerushwa katika anga la nje lililo nje ya angahewa ya dunia. Majina mengine yaliyokuwa kawaida ni "kosmonavti" (Kirusi космонавт) kwa wanaanga Warusi na "astronauti" (Kiing. astronaut) wa wanaanga kutoka Marekani. Wachina wametumia neno "taikonauti".

Mwanaanga wa kwanza katika historia ya binadamu alikuwa Mrusi Yuri Gagarin kutoka Umoja wa Kisovyeti aliyerushwa tarehe 12 Aprili 1961 kwa chombo cha angani Vostok akizunguka dunia lote mara moja katika muda wa dakika 108.

Alifuatwa 5 Mei 1961 na Alan Shepard kutoka Marekani aliyetumia chombo cha angani cha Mercury .

Mwanamke wa kwanza angani alikuwa Mrusi Valentina Tereshkova mwaka 1963.

Wanaanga wa kwanza waliofika kwenye uso wa mwezi walikuwa Wamarekani Neil Armstrong na Buzz Aldrin tar. 20 Julai 1969.

Hadi machi 2008 jumla ya watu 477 kutoka nchi 39 walifika kwenye kimo cha kilomita 100 juu ya uso wa dunia ambacho ni kimo ambako anga la nje linaanza kulingana na maelezo ya Shirikisho la Kimataifa kwa Usafiri wa Angani (Fédération Aéronautique Internationale (FAI)).

Kati ya hawa ni 24 waliofika mbali zaidi kuliko kilomita 2,000 juu ya uso wa dunia hadi njia ya mwezi kwenye anga.

Mwanaanga aliyekaa muda mrefu angani alkuwa Mrusi Sergei Krikalyov aliyefika angani mara sita akakaa jumla ya siku 803, masaa 9 na dakika 39 kwenye anga la nje.