Kiserbokroatia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 67: Mstari 67:
[[sr:Српскохрватски језик]]
[[sr:Српскохрватски језик]]
[[sv:Serbokroatiska]]
[[sv:Serbokroatiska]]
[[tg:Забони cербу xорватӣ]]
[[tg:Забони сербу хорватӣ]]
[[tr:Sırp-Hırvatça]]
[[tr:Sırp-Hırvatça]]
[[ug:سېربو-كرودىيىلىكلەر تىلى]]
[[ug:سېربو-كرودىيىلىكلەر تىلى]]

Pitio la 18:24, 3 Aprili 2010

Kiserbokroatia (2005)

Kiserbokroatia iliyoitwa pia Kikroatoserbia (halafu pia "Kiserbia au Kikroatia" na "Kikroatia au Kiserbia" - srpskohrvatski au cрпскохрватски au hrvatskosrpski au hrvatski ili srpski au srpski ili hrvatski) ilikuwa lugha rasmi ya Yugoslavia pamoja na Kislovenia na Kimasedonia.

Katika Ufalme na baadaye jamhuri ya Yugoslavia iliunganisha lahaja za karibu za Wakroatia, Waserbia na Wabosnia. Ilikuwa mpango wa kuunda lugha sanifu ya kisasa na kujenga umoja wa kitaifa.

Kufuatana na tamaduni mbalimbali katika Yugoslavia iliandikwa kwa alfabeti ya Kikirili upanda wa Mashariki katika eneo la Serbia na kwa alfabeti ya Kilatini upande wa Magharibi katika eneo la Kroatia.

Baada ya kuporomoka kwa Yugoslavia tangu 1991 maeneo yake yaliendelea kama nchi za pekee. Kila nchi kati ya Serbia, Kroatia na Bosnia-Herzegovina ilianza kudai ya kwamba lugha ya watu wake ni lugha ya pekee. Neno na wazo la "Kiserbokroatia" ilifutwa kati ya wasemaji wa lugha baada ya kipindi cha uadui na vita za wenyewe kwa wenyewe.