Dola Takatifu la Kiroma : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: no:Det tysk-romerske rike
d roboti Badiliko: hif:Holy Roman Samrajya
Mstari 75: Mstari 75:
[[he:האימפריה הרומית הקדושה]]
[[he:האימפריה הרומית הקדושה]]
[[hi:पवित्र रोम साम्राज्य]]
[[hi:पवित्र रोम साम्राज्य]]
[[hif:Holy Roman Empire]]
[[hif:Holy Roman Samrajya]]
[[hr:Sveto Rimsko Carstvo]]
[[hr:Sveto Rimsko Carstvo]]
[[hu:Német-római Birodalom]]
[[hu:Német-római Birodalom]]

Pitio la 11:33, 1 Aprili 2010

Dola Takatifu la Kiroma si sawa na Dola la Roma la Kale.
Ramani ya Dola Takatifu la Kiroma yaonyesha mikoa yake
Maeneo ya Dola Takatifu la Kiroma pamoja na mipaka ya nchi za kisasa

Dola Takatifu la Kiroma (Kijerumani: Heiliges Römisches Reich, Kilatini: Sacrum Romanum Imperium) ilikuwa jina la Ujerumani kwa wakati kati ya takriban 1000 na 1806. Lakini dola hili lilikuwa pia na maeneo makubwa licha ya Ujerumani pamoja na Austria kama Italia ya Kaskazini, Ubelgiji, Uholanzi na Ucheki. Mipaka yake yalibadilika mara kadhaa katika karne nyingi za kuwako kwake.

Tabia za Dola

Maneo haya yote yaliunganishwa chini ya Kaisari aliyekuwa pia mfalme wa Wajerumani. Maeneo haya yalikuwa na kiwango kikubwa cha kujitegemea yakitawaliwa na makabaila wa ngazi mbalimbali, maaskofu wa kanisa katoliki au yakiwa miji huru.

Halikuwa dola la kisasa na vyombo vya dola vilikuwa vichache. Kaisari alitegemea hasa mali yake ya binafsi pamoja na haki ya kuthebitisha watu waliopokea vyeo mbalimbali. Tangu 1438 hadi 1806 cheo cha Kaisari kilibaki katika familia ya Habsburg waliotawala Austria.

Chanzo baada ya Karolo Mkuu

Asili ya dola lilikuwa milki ya Karolo Mkuu aliyefaulu kuunganisha Ujerumani, Ufaransa na Italia chini yake. Mwaka 800 alipokea cheo cha Kaisari wa Roma kutoka mkono wa Papa Leo III. Hatua hii ilichukuliwa kama kuendelezwa kwa Dola la Roma la Kale katika magharibi ya Ulaya hata kama hali halisi milki ya Karolo ilikuwa milki ya Wafranki na Wagermanik wengine na taasisi zote za Roma ya Kale zilikuwa zimeshakwisha kabisa katika magharibi ya Ulaya. Yaliyobaki ya Roma ya Kale yaliendelea katika mashariki kwa umbo la Milki ya Bizanti. Lakini makaisari walijenga hoja la "translatio imperii" (kilatini: ukabidhi wa mamlaka) la kuwa mamlaka ya Kaisari yalikuwa na Waroma wa Kale na sasa yalikabidhiwa kwa Wajerumani.

Karolo aligawa urithi wake kati ya wanake na hii ilikuwa chanzo cha Ufaransa upande wa magharibi na Ujerumani upande wa mashariki. Cheo cha Kaisari kiliendelea upande wa mashariki. Hivyo Ufaransa iliendelea kuwa ufalme wa nchi moja lakini upande wa mshariki Wajerumani waliunganishwa pamoja na watu jirani chini ya Kaisari aliyekuwa pia mkuu wa Italia ya Kaskazini, Bohemia (Ucheki) na sehemu mbalimbali ambazo leo hii ni ama Ufaransa au Ubelgiji na Uholanzi.

Mjerumani wa kwanza aliyepokea ukaisari kutoka kwa papa wa Roma alikuwa Otto I mwaka 962. Dola likaendelea hadi 1806 wakati Napoleon alipoifuta. Jina la "Dola Takatifu la Kiroma" lilianza kutumiwa tangu 1100 likaitwa baadaye pia "Dola Takatifu la Kiroma la Wajerumani".

Matatizo ya Dola

Hadi karne ya 13 dola lilikuwa na nguvu. Baadaye maeneo ndani yake yaliongeza kiwango cha kujitawala. Kila Kaisari alichaguliwa na kamati ya makabaila na watemi wakuu. Hapa Makaisari walipaswa kuahidi kabla ya uchaguzi ya kwamba wataheshimu haki ya makabaila juu ya maeneo yao. Mwishoni maeneo yalikuwa kama nchi huru kabisa yaliyoendelea kujitawala, kuendesha vita dhidi ya majirani kufuata siasa zao. Dola lilikuwa mwishoni za zaidi ya maeneo 300 ya kujitegemea; mengine makubwa kama Austria na Prussia, mengine madogo mno yenye eneo la mji mmoja tu.

Tangu karne ya 16 dola halikuwa na uwezo tena kufuata siasa ya pamoja kwa nje isipokuwa dhidi ya Waturuki Waosmani walioshambulia mara mbili Vienna mji mkuu wa makaisari 1529 na 1683. Lakini vita za kuwasukuma Waturuki watoke katika maeneo ya Ulaya ya kusini-mashariki waliyowahi kuvamia viliendeshwa na Kaisari kama mkuu wa Austria bila msaada wa dola takatifu.

Dola lilifaulu kwa kiasi fulani kutunza amani au angalau kupakana vita kati ya maeneo yake. Isipokuwa Vita ya Miaka 30 kati ya 1618 na 1648 ilionyesha uwezo mdogo wa dola na karibu theluthi moja ya wakazi wa Ujerumani walikufa.

Tangu karne ya 17 majirani kama Ufaransa na Sweden walijiingiza zaidia na zaidi katika siasa ya Ujerumani na maeneo makubwa kama Prussia hayakujali tena maazimio ya Kaisari. Dola Takatifu likaendelea kudhoofika.

Vita za Napoleon zilimaliza mabaki yake.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dola Takatifu la Kiroma kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA