Alizeti : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 51: Mstari 51:
[[bg:Слънчоглед]]
[[bg:Слънчоглед]]
[[bn:সূর্যমুখী]]
[[bn:সূর্যমুখী]]
[[bo:ཉི་མ་མེ་ཏོག​]]
[[bo:ཉི་མ་མེ་ཏོག]]
[[ca:Gira-sol]]
[[ca:Gira-sol]]
[[cs:Slunečnice roční]]
[[cs:Slunečnice roční]]

Pitio la 21:43, 14 Machi 2010

Alizeti

Alizeti (Helianthus annuus) ni mmea unaodumu mwaka mmoja mwenye ua kubwa. Asili yake iko Amerika lakini imeenea pande nyingi za dunia.

Umbo na ua

[[1]] Alizeti inafikia urefu hadi mita 3 na ua lake upana hadi 30 cm.

Ua lake hali halisi ni "kichwa" au mkusanyiko ya maua madogomadogo yanayokaa kwa pamoja kama duara juu ya kombe kubwa. Maua madogo ya nje huonekana kama petali juwa kubwa zaidi na kuonyesha rangi ya manjano, wakati mwingine hata ya machungwa. Yale maua petali huzai mbegu. Kila ua mdogo ndani ya duara huwa na mbegu. Mbegu huwa na ganda gumu na ndani yake uko mbegu mwenyewe mwenye kiwango kikubwa cha mafuta.

Matumizi

Kiasili alizeti inapatikana katika Amerika. Maindio walipanda ua katika bustani zao. Wahispania walileta mbegu Ulaya baada ya kufika Amerika na mwanzoni mme ulipandwa kama ua la mapambo kwenye bustani.

Baadaye kiwango kikubwa cha mafuta ndani ya mbegu zake kilitambuliwa kikawa mme muhimu cha kuzaa mafuta.

Kufuata jua

Jua linapochomoza maua mengi ya alizeti hugeukia mashariki jua linapotokea, na wakati wa mchana huendelea kulifuata jua mpaka magharibi hurudi katika uelekeo wa mashariki tena. Mwendo huu, "heliotropism", huratibiwa na seli ziitwazo ‘pulvinus’ sehemu iliyo huru kuzunguka chini kidogo tu ya chipukizi. Hatua ya chipukizi inapo isha shina hukomaa na mmea hupoteza uwezo wake wa kuzunguka tena kulifuata jua. Mmea huganda kuelekea ( mara nyingi) upande wa mashariki. Majani na shina hupoteza rangi yake ya kijani. Mimea ya pori jamii ya alizeti huwa haizunguki kufuata jua, japo majani yake hufuata jua maana yao huelekea upande wowote pindi yanapokomaa.


Historia

[[2]] [[3]] Mmea huu una asili ya katikati ya Amerika. Wataalamu wamekadiria kuwa ulianza kulimwa sana huko Meksiko, mnamo mwaka 26000 KK na pia huko bonde la mto Mississippi. Mifano ya mimea iliyotolewa Meksiko imeonekana huko Tennessee, Marekani pia, ikionesha kuwa pale tangu 2300K.K.[4] Watu wengi wanatumia mmea wa alizeti kama ishara ya nguvu na utakatifu wa jua, hasa wale wa alizeti kama ishara ya nguvu na utakatifu wa jua. Hasa wale wa Aztecs na Otomi wa Meksiko na kusini mwa Amerika. Francisco Pizarro alikuwa mtu wa kwanza kutoka Ulaya kuuona mmea wa alizeti huko Peru. Taswira ya dhahabu ya mmea na mbegu zake zilichukuliwa na kupelekwa Hispania mnamo karne ya 16. Baadhi ya watafiti wanasema kuwa Hispania iliwekewa vikwazo vingi kilimo cha alizeti kutokana na imani ya dini imayoambatana na mmea huo. [5] Kufikia karne ya 18, matumizi ya mafuta ya alizeti yalikuwa maarufu mno, hasa kwa waumini wa kanisa la Russia la Orthodox kwa sababu mafuta ya alizeti yalikuwa miongoni mwa vitu vichache vilivyo kuwa vinaruhusiwa kutumika wakati wa kwaresma.


Kilimo na matumizi

Kukua vizuri mmea wa alizeti unahitaji jua la kutosha. Hakuna vyema kwenye arthi iliyo na rutuba ndogo wenye ukame mzuri na matandazo ya kutosha katika kilimo cha bidhaa mbegu hupandwa kwa umbali was m 45 na kinaacha 2.5. mbegu yam mea huu, alizeti, huliwa kama chakula cha kutafuna baada ya kuokwa/ kukaushwa, pamoja au bila ya chumvi. Huko ujerumani hutumika kutengenezea mikate. Alizeti pia ni chakula cha ndege na hutumika kwenye mapishi moja kwa moja na wakati wa kuandaa saladi. Mafuta ya alizeti yanayokamuliwa kutoka kwenye mbegu za alizeti hutumika kupikia, mafuta ya kutunzia vitu na huzalisha siagi na dizeli ya mimea. Sababu yana gharama ndogo kuliko mafuta ya mizeituni. Kuna mimea mingi ya jamii ya alizeti yenye aina mbalimbali na viwango mbalimbali vya mafuta.mashudu yanayobaki baada ya kukamua mafuta hutumika kulishia mifugo kama chakula, alizeti pia huweza kuzalisha mpira.

Alizeti pia hutumika kufyonza kemikali hatari kutoka ardhini kama vile urani na walitumika katika kuondoa madini ya urani ardhini baada ya janga la kinyuklia lililotokea huko Chernobyl.

Ukubwa

Mimea ya alizeti hukua kufuata kimo cha mita 1.5, mpaka 3.5. Wana sayansi wameripoti kuwa mwaka 1567, kuna mualizeti ulikuwa kufikia kimo cha mita 12 huko Padua. Mbegu zake zilipo pandwa maeneo mengine zilitoa mimea yenye urefu wa mmita 8, kwenye maeneo kama vile madvid, hivi karibuni maeneo mengine kama vile Uholanzi na Ontario, Canada nao wamefanikiwa kukuza mimea hiyo yenye urefu wa mita 8.

Alama za utamaduni

[[6]]

Alizeti iko ndani ya nembo la jimbo la Kansas, huko Marekani, na katika nembo la mji wa Kitakyushu, Japani.
Mmea wa alizeti hutumika kama alama ya ujamaa na demokrasia ya ujamaa. Hutumiwa na wafuasi wa itikadi ya Vegani.
Ua la mmea wa alizeti ndio ua la kitaifa nchini Ukraine.