Pate : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d robot Modifying: fr:Pate (île)
d robot Adding: de:Pate (Insel)
Mstari 14: Mstari 14:
[[Category:Waswahili]]
[[Category:Waswahili]]


[[de:Pate (Insel)]]
[[en:Pate Island]]
[[en:Pate Island]]
[[fr:Pate (île)]]
[[fr:Pate (île)]]

Pitio la 21:02, 7 Machi 2007

Ramani ya kisiwa cha Pate (Kenya)

Pate ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa ya Lamu mbele ya pwani la Kenya katika Bahari Hindi. Pate ni kisiwa ambacho ni karibu na Somalia. Wakati ya maji kujaa Pate inagawanywa katika sehemu mbili kwa mtaro wa bahari karibu na Siyu; wakati wa maji kupwa mtaro huwa ni pakavu.

Pate ilikuwa kati ya mahali pa kwanza pa kutembelewa na wafanyabiashara Waarabu, labda kuanzia karne ya 7 BK. Inawezekana ilikuwa tayari kati ya mahali palipotajwa katika taarifa za kale kuhusu Azania kama vile Periplus ya Bahari ya Eritrea.

Kisiwa cha Pate kilikuwa mahali pa miji muhimu ya Waswahili Pate, Siyu na Faza iliyoshindana na mji wa Lamu juu ya kipaumbele katika funguvisiwa. Katika karne ya 19 BK umuhimu wa miji hii ilirudi nyuma.

Kisiwa kilikuwa sehemu ya dola la Usultani ya Zanzibar katika karne ya 19.

Siku hizi Faza ni kijiji kikubwa cha Pate penye hospitali ndogo, polisi, nyumba ya wageni, shule ya sekondari na maduka. 2004 palikuwa na gari moja tu kisiwani ni gari la hospitali.