The Matrix : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 112: Mstari 112:
[[gl:The Matrix]]
[[gl:The Matrix]]
[[he:מטריקס]]
[[he:מטריקס]]
[[hi:द मेट्रिक्स]]
[[hr:Matrix]]
[[hr:Matrix]]
[[hu:Mátrix (film)]]
[[hu:Mátrix (film)]]

Pitio la 12:53, 31 Januari 2010

The Matrix
Kasha ya filamu Matrix
Kasha ya filamu Matrix
Imeongozwa na Wachowski brothers
Imetungwa na Wachowski brothers
Imetaarishwa na Joel Silver
Nyota Keanu Reeves
Laurence Fishburne
Carrie Anne Moss
Hugo Weaving
Joe Pantoliano
Gloria Foster
Muziki na Don Davis
Imehaririwa na Zach Staenberg
Imesambazwa na Warner Bros
Village Roadshow Pictures
Muda wake dk. 136
Imetolewa tar. 31 Machi, 1999
Nchi Marekani
Kanada
Lugha Kiingereza

The Matrix ni filamu ya kupigana na yenye uzushi wa kisayansi, ambayo ilitengenezwa mwaka wa 1999. Filamu ilitungwa na kuongozwa na Wachowski Brothers. Washiriki wakuu katika filamu hii ni Keanu Reeves, Laurence Fishburne, Carrie Anne Moss na Hugo Weaving. Mhusika mkuu katika filamu hii ni Neo (Keanu Reeves).

Filamu ilitolewa rasmi mnamo tarehe 31 Machi ya mwaka wa 1999 katika nchi ya Marekani, na ni toleo la kwanza kutoka katika mfululizo wa filamu za Matrix. Filamu imepokea Tuzo nne za Academy.

Njama

Muhtasari wa filamu

Mtu mmoja aitwaye Morpheus (Laurence Fishburne) anamwonyesha Neo Matrix ni kitu gani. Matrix ni program ya kompyuta ambao ni dunia ya uongo. Program hiyo ya kompyuta inawafanya watu kufikiria kwamba wanaishi katika dunia ya ukweli. Mashine imetengeneza program ya Matrix.

Matrix ni program ya kompyuta inayopumbaza watu na inatumia miili yao ili kujipatia nishati. Kabla ya muvi, Neo anaonekana kuwa anaishi katika program ya kompyuta ya Matrix. Kisha, Neo anagundua kuwa anaishi katika maisha ya uongo ndani ya Matrix.

Neo analazimika kupigana na Matrix ili aweze kuwaweka wanadamu huru. Na akajaribu kuwaeleza watu wote wanaishi katika Matrix kwamba yale maisha wanayoishi si ya kweli.

Mwanzoni mwa filamu kuonekana mtu mmoja aitwaye Thomas Anderson (Keanu Reeves) anafanya kazi katika kampuni ya kompyuta. Akiwa katika mtandao wa internet, Thomas Anderson anaona ujumbe unaomwambia kwamba Thomas Anderson jina lake ni Neo.

Usiku mmoja, alikutana ujumbe wa ajabu katika kompyuta yake. Ujumbe huo ulikuwa ukisema: "mfuate huyu sungura mweupe." Baada ya muda mchache, akatokea mwanamke mmoja aliyejichora picha ya sungura mweupe katika bega lake anagonga mlango wa chumba cha Neo. Neo akaona mchoro ule wa sungura mweupe.

Kwakuwa Neo anaukumbuka ule ujumbe aliyopata kutoka katika kompyuta yake, Neo akaamuwa kumfuata mwanamke huyo. Mwanamke huyo alimwongoza Neo mpaka katika kilabu ya muziki. Akakutana na mwanamke aliyemtumia ujumbe ule wa kumfuata yule sungura mweupe.

Mwanamke huyo jina lake ni Trinity. Trinity anafahamu kuwa Neo anaona kama maajabu juu ya mambo yale yaliyotokea kwa muda ule. Mwanamke huyo akamweleza Neo kwamba Matrix wanamsaka vibaya mno.

Siku iliyofuata

Neo akiwa bado anayafanyia kazi yale maelezo aliyoambiwa jana na yule mwanamke, ghafla akaletewa kufurushi ambacho ndani yake kuna simu ya mkononi. Baada ya muda mchache simu ikaita. Aliyepiga simu alikuwa Bw. Morpheus.

Morpheus na Trinity ni marafiki. Morpheus akamweleza Neo kwamba kama wewe ni (Neo) basi upo hatarini. Ghafla watu wawili waliovaa suti nyeusi wanakuja na kumvamia Neo na kisha kumkamata. Morpheus akamwambia Neo akatoroke kutoka katika jengo hilo kwa kupitia dirishani. Neo akawa anaogopa sana kuruka dirishani hapo kwani jengo lilikuwa refu sana.

Na ikapelekea Neo kushindwa kuruka katika jengo hilo, hivyo watu hao waliovaa suti nyeusi wakafanikiwa kumtia nguvuni Neo. Watu hao wakamchukua Neo hadi katika jengo lao, na wakaanza kumwulia maswali kadha wa kadha. Neo yeye alifikiri kuwa wale ni maofisa wa polisi, lakini wao hawakuwa maofisa wa polisi.

Watu hao ni program mashine kutoka duniani, wanaitwa “Ma-agent”. (Agent ni neno la kweli. Ma-agent ni wakala maalum wa polisi).

Baada ya maswali mengi watu hao walimwachia huru Neo, mara tu wanamwachia huru Trinity akatokea. Akamwamuru Neo aiingie katika gari lake. Trinity aliondoka na Neo ilikwenda kuonana na Morpheus. Morpheus ni mtu anayejua siri ya Matrix. Morpheus akamweleza Neo, “Matrix wapo kila sehemu.

Na Matrix wametuzunguka sisi wote, na hata sasa katika chumba hiki pia wapo. Unaweza kuona hilo mara tu uangalipo nje ya dirishani lako na pale uwashapo televisheni yako. Unaweza ukahisi hilo pale uendapo kazini, unapoenda kanisani, na unapolipa nauli ya taxii.

Matrix ni dunia iliyovutwa machoni mwako (sawa na shuka ambalo watoto hulitumia kujifichia) yaani inamaana ya kukupambaza na ukweli uliopo (kuficha ukweli juu yako).”

Morpheus akampa Neo chaguo. Endapo Neo atachukua kidonge cha buluu, inamaana kwamba hamna atakachojua. Na hato jua lolote kuhusu Matrix. Na Neo ataendelea kuishi katika Matrix, lakini atakuwa muda wote yeye hana raha. Na endapo Neo atachukua kidonge chekundu, atatambua ukweli wote kuhusu Matrix. Neo alikibali kula kidonge chekundu, kilichotokea baada ya kula kidonge.....

Washiriki

Kutoka kushoto ni: Agent Jones, Agent Smith na Agent Brown.
  • Laurence Fishburne kacheza kama Morpheus: humu alikuwa kiongozi wa wana Nebuchadnezzar. na mmoja kati ya rafiki wa Neo.
  • Carrie Anne Moss kacheza kama Trinity: Huyu na Morpheus, na mmoja kati wana Nebuchadnezzar na ndiyo kipenzi pekee wa Neo.
  • Hugo Weaving kacheza kama Agent Smith: Huyu ndiyo jangili mkuu na ndiyo Matrix mama, mwenye lengo la kuamgamiza wana wa Zion na kuzuiya wanadamu wote wanaotaka kuhondosha harakati za Matrix.
  • Joe Pantoliano kacheza kama Cypher: Huyu ni mmoja wa watu wa Morpheus, lakini aliwasaliti wenziwe (Nebuchadnezzar) na kuwa mmoja kati wa wana-Matrix, na akaua watu watatu wa Neo, lakini mwishowe akaangamizwa na Bw. Tank."
  • Julian Arahanga kacheza kama Apoc: Ni mmoja kati ya wana Nebuchadnezzar.
  • Anthony Ray Parker kacheza kama Dozer: Ni mwanadamu wa kawaida, yaani hakuwa mmoja wa Nebuchadnezzar, lakini yeye ndiye alikuwa rubani wa ndege yao.
  • Marcus Chong kacheza kama Tank: Huyu ni ndugu wa Dozer, nae alikuwa mwanadamu asilia na mtaalam wa kuwaendesha na kutoa mwongozo kwa wana wa Nebuchadnezzar.
  • Matt Doran kacheza kama Mouse: Mmoja wa Nebuchadnezzar na ndiyo mprogramuji wa wana wa Nebuchadnezzar.
  • Gloria Foster kacheza kama Oracle: Ni mwanamama aliye uhamishoni mwa Matrix( nae ni Matrix lakini wamemtenga), na anaamua kuwasaidia wa wa Nebuchadnezzar kwa kutumia hekima yake na uweze wake wa kuweza kutabiri jambo lijalo kwa siku za usoni.
  • Belinda McClory kacheza kama Switch: Ni mmoja wa wana wa Nebuchadnezzar.
  • Paul Goddard kacheza kama Agent Brown: Mmoja katika ya Ma-Agent wa Matrix.
  • Robert Taylor kacheza kama Agent Jones: Agent wa pili wa wana Matrix.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu: