Kimondo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: mr:उल्का
Mstari 58: Mstari 58:
[[da:Meteoroid]]
[[da:Meteoroid]]
[[de:Meteoroid]]
[[de:Meteoroid]]
[[el:Μετέωρο]]
[[en:Meteoroid]]
[[en:Meteoroid]]
[[eo:Meteoroido]]
[[eo:Meteoroido]]
Mstari 66: Mstari 65:
[[fi:Meteoroidi]]
[[fi:Meteoroidi]]
[[he:מטאורואיד]]
[[he:מטאורואיד]]
[[hi:उल्का]]
[[hr:Meteoroid]]
[[hr:Meteoroid]]
[[hu:Meteoroid]]
[[hu:Meteoroid]]
Mstari 90: Mstari 90:
[[sv:Meteoroid]]
[[sv:Meteoroid]]
[[th:สะเก็ดดาว]]
[[th:สะเก็ดดาว]]
[[uk:Метеороїд]]
[[vi:Thiên thạch]]
[[vi:Thiên thạch]]
[[zh:流星体]]
[[zh:流星体]]

Pitio la 12:58, 26 Januari 2010

Vimondo vinavyong'aa angani; picha imechukuliwa kwa muda wa dakika kadhaa na kuonyesha vimondo kadhaa vilivyoonekana katika kipindi hiki. Nyota hazionekani kama nukta tena lakini kama mistari mifupi kutokana na mwendo wa dunia na anga katika muda wa kupigiwa kwa picha.

Vimondo (pia: meteori au meteoridi) ni magimba madogo ya angani yanayozunguka jua. Yanaweza kuanguka duniani yakionekana kama moto angani.

Ukubwa

Ukubwa wa kimondo ni kuanzia punje la mchanga hadi kufikia kipenyo cha mita kadhaa. Hivyo kimondo ni kidogo kuliko asteoridi na kikubwa kushinda vumbi la angani.


Kimondo hiki cha chuma kilipatikana China

Kugonga angahewa ya dunia

Mzunguko wa kimondo unaweza kuingiliana na njia ya dunia au sayari nyingine. Kama kimondo kikilikaribia gimba la angani kubwa zaidi kinavutwa nalo.

Kikikaribia mno dunia yetu kinaingia katika angahewa na kuanguka chini kwa kasi kubwa sana. Njiani kinapashwa moto kutokana shindikizo la hewa dhidi yake. Kiasi cha joto kinatosha kuchoma kimondo kidogo kabisa hewani. Hii inaonekana kwa macho matupu kama mstari wa moto angani. Kama kimondo ni kubwa zaidi ni sehemu zake za nje tu zinazochomwa na kiini kinagonga uso wa dunia.

Kati ya vimondo kumi vikubwa kabisa duniani ambavyo mabaki yao yanaonekana ni Kimondo cha Mbozi nchini Tanzania.

Hatari za vimondo ?

Vimondo ni hatari kwa vyombo vya angani kwa sababu ya kasi kubwa. Hata punje dogo laweza kusababisha uharibifu mwingi.

Duniani kuna pia hatari fulani lakini si kubwa hali halisi. Katika miaka yote ya karne ya 20 kuna taarifa 21 pekee za nyumba kugongwa na kimondo.

Katika karne ya 20 kuna taarifa zifuatazo kuhusu watu walioathiriwa na vimondo:

  • 5 Septemba 1907 Weng-li, China - familia yote kuuawa
  • 30 Juni 1908 Tunguska, Siberia - Moto porini, watu wawili kuuawa
  • 28 Aprili 1927 Aba, Japan - binti kujeruhiwa na kimondo
  • 08 Desemba 1929 Zvezvan, Yugoslavia - Kimondo kugonga arusi, mmoja kuuawa
  • 16 Mei 1946 Santa Ana, Meksiko - Nyumba kuharibiwa, watu 28 kujeruhiwa
  • 30 Novemba 1946 Colford, UK - simu kuharibiwa, mvulana kujeruhiwa
  • 28 Novemba 1954 Sylacauga, Alabama, USA - kimondo cha kilogramu nne kugonga nyumba, mama kujeruhiwa
  • 14 Agosti 1992 Mbale, Uganda - Vimondo 48 kuanguka, mvulana kujeruhiwa
Kasoko huko Arizona (Marekani) kutokana na mgongano wa kimondo

Mgongano na vimondo vikubwa

Lakini kuna hatari moja kubwa kwa maisha yote duniani. Wataalamu huamini ya kwamba kila baada ya miaka maelfu hadi malakhi kadhaa kimondo kikubwa au zaidi asteroidi inaweza kugonga dunia. Nishati ya mgongano wa aina hii inaweza kuwa kubwa sana na kuleta uharibifu mwingi.

Tokeo la Tunguska tar. 30 Juni, 1908 katika pori la Siberia liliangusha miti milioni 60 kwenye eneo la kilomita za mraba 2000. Wataalamu walio wengu huamini ya kwamba lilisababishwa na kimondo. Kama lingetokea juu ya mji wa kisasa kuna hofu ya vifo vingi sana.

Kuna pia kasoko kadhaa zilizosababishwa na vimondo. Vimondo vikubwa sana viliovyoweza kusababisha kasoko kubwa vinatokea kila baada ya miaka mamilioni. Lakini vina hatari ya kuua kiasi kikubwa cha viumbe vyote katika nchi au hata duniani.

Viungo vya Nje


Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimondo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.