Meno : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: en:Tooth (human)
d roboti Nyongeza: sco:Tuith; cosmetic changes
Mstari 9: Mstari 9:

== Muundo wa Jino ==
== Muundo wa Jino ==
[[File:Tooth-anatomy.gif |thumb|250px|right|Muundo wa jino]]
[[Picha:Tooth-anatomy.gif |thumb|250px|right|Muundo wa jino]]

Meno hukaa kwa uthabiti ndani ya [[vitundu vya mataya]]. Kila jino lina sehemu mbalimbali. Sehemu ambayo huonekana kinywani ni [[kichwa cha jino]], na sehemu iliyomo ndani ya taya ni [[shina la jino]]. Karibu jino zima ni la [[pembe]]. Kichwa chake ni cha ufupa mgumu sana wenye rangi nyeupe ya kung’aa, nacho kwa [[lugha ya kitaalam]] huitwa [[enamel]]. Kazi yake ni kulinda [[pembe ya ndani]]. Pembe ya shina hulindwa na tabaka aina ya [[saruji]] ijulikanayo kwa jina la kitaalamu kama [[cementum]].

Mstari 23: Mstari 23:
=== Kiseyeye ===
=== Kiseyeye ===

Zaidi ya kuoza kwa meno kuna ugonjwa wa [[mishipa inayozunguka meno]], ndiyo [[kiseyeye]] (Pyrrohoea). Katika ugonjwa huu [[ufizi]] unaweza kuvimba na kutoka damu ukiguswa kidogo tu, kama kwa mfano mtu anaposafisha meno yake kwa [[mswaki]]. Ugonjwa ukizidi ule mfupa unaozunguka jino utaharibika na jino litalegea na mwishowe hata kutoka lenyewe. Ugonjwa huu husababishwa na ukosefu wa [[vitamini C]] mwilini.

=== Magonjwa mengine yanayosababishwa na meno mabovu ===
=== Magonjwa mengine yanayosababishwa na meno mabovu ===
Mstari 49: Mstari 49:
* [http://users.forthnet.gr/ath/abyss/dep1151.htm Muundo wa aina za Meno]
* [http://users.forthnet.gr/ath/abyss/dep1151.htm Muundo wa aina za Meno]
* [http://library.thinkquest.org/22484/noframes/teeth_.html Aina za Meno]
* [http://library.thinkquest.org/22484/noframes/teeth_.html Aina za Meno]

[[Jamii:Biolojia]]
[[Jamii:Biolojia]]
Mstari 117: Mstari 116:
[[ru:Зубы человека]]
[[ru:Зубы человека]]
[[scn:Denti]]
[[scn:Denti]]
[[sco:Tuith]]
[[simple:Tooth]]
[[simple:Tooth]]
[[sk:Zub]]
[[sk:Zub]]

Pitio la 02:42, 11 Januari 2010

Aina za meno kinywani

Utangulizi

Uyeyusho wa chakula huanzia kinywani. Humo tunakitafuna kwa meno mpaka kiwe laini. Kuna wakaa mbili za meno. Idadi ya meno katika wakaa ya kwanza ni 20. Huanza kuota mtoto anapokuwa na umri wa miezi sita na kawaida yote huwa yamekwisha kuota mtoto anapotimiza umri wa miaka miwili. Idadi ya meno katika wakaa ya pili ni thelathini na mbili. Huanza kuota katika umri wa miaka sita, yakakamilika katika umri wa miaka 18-20. Lakini mwingine huota upesi au hukawia.

Aina za Meno

Umbo la meno hufuatana na kazi ambayo inayapasa kufanya. Meno yaliyopo katikati ya kila taya huwa na kingo kali za kukatia chakula. Haya huitwa meno ya kutatia au meno ya mbele (incisors). (meno 8 ya kukatia, katika kila taya yapo meno 4). Meno yaliyofuata meno ya kukatia ni machonge (canine). Yapo machonge 4 kwa ujumla; katika kila taya kuna machonge 2. Kazi yake ni kurarua chakula. Meno yanayofuata machonge huitwa magego madogo (premolars) (jumla ya magego madogo ni 8; na katika kila taya yapo 4); na meno yanayoyafuata hayo huitwa magego (molars) (magego yate ni 12, na katika kila taya kuna magego 6. Magego madogo na magego ni kwa kusagia chakula. Katika wakaa wa kwanza huwa hakuna magego madogo.

Muundo wa Jino

Muundo wa jino

Meno hukaa kwa uthabiti ndani ya vitundu vya mataya. Kila jino lina sehemu mbalimbali. Sehemu ambayo huonekana kinywani ni kichwa cha jino, na sehemu iliyomo ndani ya taya ni shina la jino. Karibu jino zima ni la pembe. Kichwa chake ni cha ufupa mgumu sana wenye rangi nyeupe ya kung’aa, nacho kwa lugha ya kitaalam huitwa enamel. Kazi yake ni kulinda pembe ya ndani. Pembe ya shina hulindwa na tabaka aina ya saruji ijulikanayo kwa jina la kitaalamu kama cementum.

Katikati hasa ya cementum na mfupa wa taya kuna utando, ambao unasaidia kukuza jina katika kitundu chake, nao (utando huo) hulingana na ufizi. Ndani ya jino mna mvungu wenye neva na mishipa ya damu. Neva pamoja na mishipa ya damu huingia katika mvungu penye ncha ya shina la jino.

Magonjwa ya Meno

Kuoza kwa meno

Chakula cha hatari kwa meno ni baadhi ya kile chenye asili ya unga. Kikiachwa kinywani huganda katika meno; hapo meno hupata kuwa mororo na mahali pale uharibifu utaanza. Basi vijidudu vilivyomo kinywani hushambulia mahali pale na hatimaye hutoboa kitundu. Ukubwa wa kitundu hiki utaongezeka polepole. Mwishowe kitafika mpaka mvungu wenye neva, ndipo yanapotokea maumivu makali. Hatimaye neva itaoza na kufa kabisa. Hapa maumivu hutulia kabisa. Lakini usikubali kudanganywa. Kwa njia ya mvungu hata nafasi inayozunguka ncha ya jino itashambuliwa, na vijidudu vitaenea hadi kwenye utando wa ule mfupa na hatimaye kusababisha jipu na madhara mengine kinywani.

Kiseyeye

Zaidi ya kuoza kwa meno kuna ugonjwa wa mishipa inayozunguka meno, ndiyo kiseyeye (Pyrrohoea). Katika ugonjwa huu ufizi unaweza kuvimba na kutoka damu ukiguswa kidogo tu, kama kwa mfano mtu anaposafisha meno yake kwa mswaki. Ugonjwa ukizidi ule mfupa unaozunguka jino utaharibika na jino litalegea na mwishowe hata kutoka lenyewe. Ugonjwa huu husababishwa na ukosefu wa vitamini C mwilini.

Magonjwa mengine yanayosababishwa na meno mabovu

Licha ya magonjwa meno, hata magonjwa mengine yanaweza kutokea. Mara nyingi vijidudu vya jipu huingia moja kwa moja katika njia ya damu, au pengine usaha unaomezwa pamoja na vijidudu huweza kuanzisha ugonjwa wa kuvimba katika sehemu nyingine za mwili.

Utunzaji wa meno

Inampasa kila mtu kusafisha meno yake baada ya kula na kuondoa vipande vyote vya chakula vinavyobaki hasa kati ya jino na jino. Wakati mwingine ulio bora kwa kusafisha meno kabla ya kwenda kulala. Ili ufanikiwe kusafisha meno vizuri tumia mswaki; na ili kuondoa vipande vya chakula vilivyomo kati ya jino na jino tumia kijiti chenye ncha kali au kilichochongeka. Wakati ugonjwa wa meno unapoanza, ikiwa daktari wa meno yuko katika mtaa au kijiji chako, umwendee ili azibe tundu la jino lako. Jino lolote bovu lisiloweza kutibiwa tena inafaa ling’olewe ili lisiweze kuambukiza ugonjwa katika sehemu nyingine za mwili.

Angalia Pia

Marejeo

  • Roberts, M. (2000). Advanced Biology, Nelson, London.
  • Franks, A. S. T. (1973). Geriatric Dentistry, Oxford

Viungo vya nje