Uholanzi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: pcd:Bos-Péis
d roboti Nyongeza: dv:ނެދަލޭންޑު
Mstari 159: Mstari 159:
[[Jamii:Nchi za Ulaya]]
[[Jamii:Nchi za Ulaya]]
[[Jamii:Uholanzi|*]]
[[Jamii:Uholanzi|*]]

[[pcd:Bos-Péis]]


[[ace:Olanda]]
[[ace:Olanda]]
Mstari 195: Mstari 197:
[[diq:Hollanda]]
[[diq:Hollanda]]
[[dsb:Nižozemska]]
[[dsb:Nižozemska]]
[[dv:ނެދަލޭންޑު]]
[[dz:ནེ་དར་ལེནཌསི་]]
[[dz:ནེ་དར་ལེནཌསི་]]
[[ee:Netherlands]]
[[ee:Netherlands]]
Mstari 284: Mstari 287:
[[pam:Netherlands]]
[[pam:Netherlands]]
[[pap:Hulanda]]
[[pap:Hulanda]]
[[pcd:Bos-Péis]]
[[pdc:Holland]]
[[pdc:Holland]]
[[pih:Dem Nethiland]]
[[pih:Dem Nethiland]]

Pitio la 22:20, 30 Desemba 2009

Koninkrijk der Nederlanden
Ufalme wa Nchi za Chini
Bendera la Uholanzi Nembo ya Uholanzi
Bendera Nembo
Hadabu ya Taifa: Je maintiendrai
(Kifaransa)
Kiswahili, Nitastahimili
Mahali pa Uholanzi
Lugha za Taifa
Kiholanzi
kwa mkoa wa Friesland: Kifrisi
Mji Mkuu Amsterdam
Makao wa Serikali Den Haag
Malkia Beatrix van Oranje Nassau
Waziri Mkuu Jan Peter Balkenende
Eneo
 - Jumla
 - % Maji

41,526 km²
18.41
Umma
 - Jumla
 - msongamano]]

16,407,476 (Julai 2005)
395/km²
GDP
 - Jumla
 - kwa kipimo cha umma

$625 bilioni
$ 30,500
Uhuru
 - Tangazwa
 - Kiriwa
Kutoka Hispania
  Julai 26, 1581
  Januari 30, 1648
Fedha Euro € EUR
Saa za Eneo UTC +1
Wimbo wa Taifa Wilhelmus
TLD mtandao .nl
Kodi ya simu 31

Uholanzi ni nchi katika Ulaya wa Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini. Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na kisima cha Aruba na Visima vya Karibi vya Uholanzi.

Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hili, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi ni chini ya bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.

Jiografia

Akifika Uholanzi kwa uwanja wa ndege wa Schiphol, msafiri atastaajabu na nchi ya tambarare. Kwa kweli, kuna sehemu zenye vilima, lakini sehemu kubwa zaidi ya Uholanzi ni tambarare. Mahali pa juu kabisa nchini ni Kilima cha Vaals, upande wa kusini wa mkoa wa Limburg, kwa 322 m. Mahali pa chini kabisa ni karibu na Nieuwerkerk aan de IJssel, mkoa wa Zuid Holland, kwa -6.76 m (mita 6.76 chini ya usawa wa wastani wa bahari).

Vipande vikubwa vya nchi vimepatwa kwa maji. Kufanya hii boma linajengwa linalozunguka ziwa au sehemu ya bahari kisha maji yanavutwa kwa bomba. Mahali kati ya boma huitwa “polder”. Mkoa mmoja wote, Flevoland, umepatwa kwa maji ya “Zuiderzee” (Bahari ya Kusini). Kwa sababu ya hii watu husema: “Mungu aliumba dunia lakini Waholanzi waliumba Uholanzi.” Hata sasa sehemu muhimu ya Uholanzi ni maji: 18%.

Boma la Oosterschelde na malango na barabara

Maboma mengine makubwa yamejengwa upande wa kusini magharibi wa nchi ili ya kuzuia maji yasienee mikoa ya Zeeland na Zuid Holland. Mradi huu huitwa “Deltawerken” au Ujenzi wa Delta. “Oosterscheldekering” au boma la mto wa Oosterschelde ni jengo linaloshangaza. Urefu wake ni 9 km na katikati yake kuna malango makubwa 62 ambayo hujifunga wenyewe kila wakati ambapo maji ya bahari yakifura zaidi ya 3 m. Barabara kuu inapitia juu ya boma hili.

Mikoa

Ramani ya Uholanzi. Nukta nyekundu zinaonyesha miji mikuu ya mikoa na nukta nyeusi zinaonyesha miji mikubwa mingine.

Uholanzi umegawanyika na mikoa 12. Kila mkoa unatawaliwa na gavana ambaye huitwa “Commissaris van de Koningin” isipokuwa yule wa Limburg ambaye huitwa “Gouverneur”. Mikoa na miji mikuu yao ni :

Mkoa Mji mkuu
Groningen Groningen
Friesland Leeuwarden
Drenthe Assen
Overijssel Zwolle
Gelderland Arnhem
Utrecht Utrecht
Flevoland Lelystad
Noord-Holland Haarlem
Zuid-Holland Den Haag (The Hague)
Zeeland Middelburg
Noord-Brabant ’s-Hertogenbosch (Den Bosch)
Limburg Maastricht


Picha ya Uholanzi iliyopigwa kutoka satellite

Miji mikubwa

Mji Wakazi
Amsterdam 742,011
Rotterdam 600,000
Den Haag 476,000
Utrecht 281,569
Eindhoven 209,399

Mito

Mito mikubwa kadhaa inaingia Uholanzi na kutiririka katika Bahari ya Kaskazini. Mto Rijn (Rhine) unaingia kwa Tolkamer upande wa mashiriki, na karibu na Nijmegen Mto Waal unajitenga ambao unachukua 70% ya maji. Mto IJssel unajitenga karibu na Westervoort na kwenda upande wa kaskazini. Mto Maas (Meuse) unaingia Uholanzi upande wa kusini wa Limburg, na karibu na Mook unageuka upande wa magharibi. Mto Schelde unaingia upande wa kusini wa Zeeland.

Trafiki

Katika Uholanzi daima ni busy sana kwenye barabara. Hii ni kwa sababu watu katika kazi asubuhi hadi jioni na kurejea. Na wanaoishi katika Uholanzi pia watu wengi, na kuifanya kazi nyingi sana.

Viungo vya nje

Historia, jiografia na siasa

Kusafiri

Viungo anuwai

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Uholanzi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi