Wikipedia:Mwongozo (Kuhariri) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
lugha
d Aliulinda "Wikipedia:Mwongozo (Kuhariri)" ([edit=autoconfirmed] (indefinite) [move=autoconfirmed] (indefinite))
(Hakuna tofauti)

Pitio la 07:15, 10 Desemba 2009

Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    
Bonyeza "hariri" kubadili makala
Bonyeza "hariri" kubadili makala

Ukitoa kurasa chache zinazolindwa, kila ukurasa una kiungo kinachosema "hariri", ambacho kinakupatia nafasi ya kubadilisha ukurasa unaotazama.

Hiki ni kipengele muhimu sana cha Wikipedia, na wote wanaruhusiwa kufanya masahihisho, kuongezea au kuondoa habari kwenye makala. Iwapo unaongeza habari fulani kwenye makala, tafadhali weka marejeo, kwa sababu habari zisizo na uthebitisho kuna uwezekano mkubwa wa kuondolewa.

Nenda kwa sanduku la mchanga na ubonyeze kiungo cha "hariri". Hii itafungua dirisha la kuhariria lililo na maandishi ya ukurasa huu. Weka kitu cha kujifurahisha au "Salam ulimwengu!", halafu Hifadhi kurasa na tazama nini ulichofanya! Kuwa mwangalifu kuhakikisha kwamba una hariri ukurasa wa sanduku la mchanga, na siyo maandishi ya ukurasa huu wa mwongozo.

Onyesha hakikisho

Moja ya vipengele muhimu cha kuanza kutumia sasa ni kitufe cha Onyesha hakikisho la mabadiliko. Jaribu kufanya uhariri kwenye sanduku la mchanga, halafu bonyeza kitufe cha Onyesha hakikisho la mabadiliko badala ya Hifadhi Kurasa. Hii inakuruhusu kuona kurasa itakavyoonekana baada ya kuhifadhi, kabla hujahifadhi. Wote twafanya makosa; kipengele hiki kinakuonyesha makosa hayo. Kutumia Onyesha Hakikisho la Mabadiliko kabla ya kuhifadhi pia inakuruhusu kujaribu kubadili miundo na maharirio mengine bila ya kupagaranyua historia ya kurasa. Usisahau kuhifadhi maharirio yako baada ya kuhakiki!

Muhtasari wa kuhariri

Kitufe cha "Onyesha hakikisho la mabadiliko" kipo upande wa kulia baada ya kitufe cha "hifadhi kurasa" na chini yake ni uga ya "kuhariri muhtasari.

Kabla hujagonga Hifadhi kurasa ni adabu nzuri kuingiza maelezo mafupi sana kuhusu kile ulichobadilisha kwenye sanduku la Muhtasari lililopo baina ya dirisha la kuhariria na kitufe cha Hifadhi kurasa. Inaweza kuwa kifupi sana; kwa mfano kama unaingiza neno "typo", watu watajua kama umefanya masahihisho ya tahajia. Pia, iwapo mabadiliko uliyoyafanya kwenye kurasa yalikuwa madogo, kama vile kusahihisha tahajia na makosa ya kisarufi, kuwa makini kutazama kisanduku cha "Haya ni mabadiliko madogo" (hii inapatikana ukiwa umeingia kwenye akaunti yako tu, basi).


Jaribu kuhariri katika sanduku la mchanga
Endelea mwongozo na Muundo