Wikipedia:Mwongozo (Muundo) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 69: Mstari 69:


Jaribu kuandika kichwa kwenye sanduku la mchanga wa ukurasa huu.
Jaribu kuandika kichwa kwenye sanduku la mchanga wa ukurasa huu.

{{-}}
<div style="float:left; align:left; margin-top: -1.5em; background-color: #f5faff; padding: .2em .6em; font-size: 130%; border: 1px solid #cee0f2;">'''Jaribu kuhariri katika [[Wikipedia:Ukufunzi (Kuhariri)/sanduku la mchanga|sanduku la mchanga]]'''</div>
<noinclude>

Pitio la 12:23, 2 Desemba 2009

Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Kupanga umbo la maandishi ni tofauti kidogo na kuandika kwenye kichakata matini (programu ya kuandika) kama vile Word, Writer na kadhalika.

Unaandika katika dirisha la uhariri. Humo huoni umbo la maandishi jinsi inavyotokea baadaye. Maana hapa hakuna kile kinachoitwa "WYSIWYG" ("What You See Is What You Get unachoona ni sawa kile kinachotokea").

Badala yake Wikipedia hutumia misimbo (codes) inayosababisha kutokea kwa maandishi manene, makubwa, madogo, ya rangi, vichwa au viungo na kadhalika. Hii ni lugha ya kompyuta ya pekee inayoitwa wikitext ikifanana na HTML lakini imerahisishwa.

Herufi koza na italiki

Misimbo inayotumika hasa kwenye wikipedia ni Herufi koza' na italiki. Yote mawili hupatikana kwa kuingiza neno / maneno kwa alama za apostrofi ('').

Unaandika Unapata
''italiki'' italiki

'''koza'''

koza

'''''koza italiki'''''

koza italiki

Kwa kawaida si lazima kutaipu apostrofi moja-moja. Unaweza kuangaza neno au maneno husika kwa puku yako na kutumia menyu (nembo dogo) juu ya dirisha la uhariri. "B" inakupa herufi koza, "I" inaleta herufi italiki.

Jina la makala ya wikipedia inatakiwa kuonekana kwa herufi koza pale inapoonekana mara ya kwanza ndani ya makala, mara nyingi kama neno / maneno ya kwanza.

Mfano: Makala ya Julius Nyerere inaanza:

"Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922..."

Herufi italiki hutumiwa kwa ajili ya majina ya vitabu, filamu au albamu za muziki. Pia kwa kuonyesha matamshi ya neno la kigeni.


Vichwa na vichwa vidogo

Vichwa na vichwa vidogo ni njia ya haraka kuboresha mpangilio wa makala. Kama maandishi ni marefu kiasi ni afadhali kuingiza vichwa hivi.

Vichwa huanzishwa kwa njia hiyo (hakuna alama kwa kazi hii kwenye menyu)

Unaandika Unapata

== Kichwa ==

Kichwa

=== Kichwa kidogo 1 ===

Kichwa kidogo 1

==== Kichwa kidogo 2 ====

Kichwa kidogo 2

Kama vichwa 4 au zaidi vimeshaingizwa katika makala sanduku ya yaliyomo inaanzishwa na programu peke yake. Tazama juu: sanduku hili limejitokeza tu bila kazi ya zioada kwa sababu kuna vichwa vinne kwenye ukurasa!

Jaribu kuandika kichwa kwenye sanduku la mchanga wa ukurasa huu.


Jaribu kuhariri katika sanduku la mchanga