Wanzilishaji wa akaunti, Warasimu, Watumiaji waliothibitishwa, Interface administrators, IP block exemptions, Wakabidhi
52,013
edits
(New page: '''Mfalme''' ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa ...) |
No edit summary |

[[Image:Form of Government.png|thumb|450px|'''Aina za serikali duniani'''
aina za [[Jamhuri]]: buluu, kijani, njano na machungwa;
'''[[Ufalme]]''':
'''nyekundu''' Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka madogo tu ya kisiasa
'''dhambarau''':Ufalme wa kikatiba, mfalme ana madaraka makubwa
'''dhambarau nyeusi''': mfalme ana madaraka yote habanwi na katiba
'''Mengine''': Utawala wa chama kimoja au kamati ya kijeshi]]
'''Mfalme''' ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa [[ufalme]]. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.
Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "[[malkia]]".
==Madaraka ya mfalme==
Madaraka ya wafalme walitofautiana kati ya nchi na nchi na kati ya kipindi na kipindi cha historia. Mifano ni:
* Mfalme wa kikatiba imekuwa hali ya kawaida katika karne ya 19 na 20 pale ambako utaratibu wa kifalme umeendelea. Mfalme hatekelezi tena shughuli za serikali. Serikali inachaguliwa na bunge kwenye msingi wa kura wa raia wote jinsi ilivyopangwa katika [[katiba]] ya nchi. Nafasi ya mfalme unafanana na ile ya [[rais]] katika [[jamhuri]]. Kuna tofauti kama mfalme ana athira katika siasa au kama cheo chake ni cha heshima tu na hana uwezo wa kuingilia kati katika kazi za bunge na serikali. Mifano yake ni wafalme wa [[Skandinavia]] au pia utaratibu wa Uingereza na nchi za [[Jumuiya ya Madola]] zisizo jamhuri. Nafasi ya mfalme iko hasa kama vikundi ndani ya bunga havikubaliani kuhusu serikali mpya na hakuna upande mwenye kura nyingi kabisa.
Wafalme wa nchi kama [[Moroko]] na [[Yordani]] wana athira kubwa zaidi.
* Mfalme mwenye mamlaka yote bila kufungwa na katiba alikuwa jambo la kawaida zamani lakini leo hii wamebaki wachache sana. Falme za aina ni [[Saudia]], [[Omani]], [[Qatar]], [[Uswazi]], [[Brunei]] na [[Bhutan]].
*Mfalme wa sehemu ya taifa tu: mifano yake ni [[Kabaka]] wa [[Buganda]] au [[Asantehene]] wa [[Ashanti]] katika [[Ghana]]. Wafalme hawa wa jadi bado wanaheshimiwa na kuwa na athira kwa sababu wanatambuliwa na watu wao hata ndani ya jamhuri kubwa zaidi kuliko eneo la kabila au kundi lao.
==Wafalme na watawala wengine==
Hakuna utaratibu sanifu mtawala gani anastahili kuitwa "mfalme". Kwa kawaida anasimamia eneo au nchi ya kujitegemea lakini wengine huweka pia mashariti kuhusu ukubwa wa eneo lake.
Kwa maeneo fulani kuna vipindi katika historia ambako si rahisi kutofautisha kati ya wafalme na watawala wadogo wengine kama [[mtemi|watemi]], [[chifu|machifu]] n.k..
Mara nyingi watawala wa Waswahili ambao hawakuwa na mamalaka nje ya eneo dogo la mji wao walijiita [[Sultani]] na Wareno waliwaita "reyes" (wafalme).
Hali hii ililingana na mifano mingine kama kati ya [[Wagiriki wa Kale]] ambako vilevile watawala wadogo juu ya miji walitumia cheo cha "mfalme".
Tazama pia: [[Kaisari]], [[Mtemi]]