Luangwa (mto) : Tofauti kati ya masahihisho
d roboti Nyongeza: hi:लुंग्वा नदी |
d roboti Nyongeza: fr:Luangwa (rivière) |
||
Mstari 31: | Mstari 31: | ||
[[en:Luangwa River]] |
[[en:Luangwa River]] |
||
[[es:Río Luangwa]] |
[[es:Río Luangwa]] |
||
[[fr:Luangwa (rivière)]] |
|||
[[hi:लुंग्वा नदी]] |
[[hi:लुंग्वा नदी]] |
||
[[nl:Luangwa (rivier)]] |
[[nl:Luangwa (rivier)]] |
Pitio la 17:29, 5 Novemba 2009
Mto wa Luangwa | |
---|---|
| |
Chanzo | Milima ya Mafinga, Zambia |
Mdomo | Mto Zambezi |
Nchi za beseni ya mto | Zambia, Malawi, Msumbiji |
Urefu | 806 km |
Kimo cha chanzo | 1,500 m |
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni | 31.6 m³/s |
Eneo la beseni (km²) | 145,700 km² |
Mto Luangwa ni mto mkubwa wa Zambia ya mashariki.
Kuna mto wa pili mdogo zaidi mwenye jina hili unaoishia katika Ziwa Kariba.
Mwendo
Luangwa ina chanzo chake katika milima ya Mafinga karibu na mpaka wa Tanzania na Malawi. Kwa jumla huelekea kusini sambamba na mpaka wa Malawi. Unapita maeneo mapana ya hifadhi za taifa za Luangwa Kaskazini na Luambe hadi Luangwa Kusini.
Takriban kilomita 500 baada ya chanzo bonde la mto linakuwa nyembamba lenye magenge makali kila upande. Kabla ya mdomo wake Luangwa ni mpaka kati ya Zambia na Msumbiji.
Mto unaishia katika Zambezi kwenye mji wa Luangwa.
Mabadiliko makubwa ya kiwango cha maji
Kiasi cha maji ndani ya mto hubadilika sana kufuatana na majira. Wakati wa ukame mto una maji kidogo na mahali pengi unapitika kwa miguu. Lakini kati ya Disemba hadi Machi wakati wa mvua katika milima ya chanzo chake na cha tawimito kuna maji mengi. Kila mwaka mwendo wa mto unaweza kubadilika kiasi kutokana na nguvu ya maji. Hii ni sababu moja ya kwamba hakuna watu wengi wanaokaa kando la mto huu.