Protini : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: scn:Prutiìna; cosmetic changes
d roboti Badiliko: az:Zülallar
Mstari 33: Mstari 33:
[[an:Proteína]]
[[an:Proteína]]
[[ar:بروتين]]
[[ar:بروتين]]
[[az:Zülal]]
[[az:Zülallar]]
[[bat-smg:Baltīms]]
[[bat-smg:Baltīms]]
[[bg:Белтък]]
[[bg:Белтък]]

Pitio la 06:28, 28 Oktoba 2009

Protini ni molekuli ndefu na sehemu za lazima katika muundo wa seli za mwili wa viumbehai. Zinajengwa na amino asidi. Protini huwajibika kwa maumbile ya seli na kushughulika usafirishaji wa dutu ndani ya seli na kati ya seli za mwili. Musuli zinaundwa pamoja na protini za pekee zenye uwezo wa kupanua na kujikaza hivyo kuweka msingi wa mwendo.

Protini zinapatikana katika wanyama, mimea, fungi na bakteria.

Protini katika chakula

Wanyama wote pamoja na binadamu huhitaji protini katika chakula chao kwa sababu hawana uwezo wa kujijengea amino asidi zote zinazohitajika kwa kujenga miili yao. Kwa sababu hiyo tunahitaji chakula chenye protini; mahitaji ya mwanadamu ni takriban gramu 1 ya protini kwa kilogramu 1 ya uzito wa mwili wake; maana mtu mwenye uzito wa kilogramu 70 anashauriwa kula gramu 70 za protini kwa siku.

Tumboni mwa binadamu na wanyama protini za chakula huvunjwa kwa asidi asidi ndani yao; kutoka hizi mwili unajenga protini mpya ya aina yake ya pekee.

Uhaba wa protini unasababisha magonjwa; uhaba mkali unaleta unyafuzi. Unyafuzi unashika hasa watoto wanaopewa chakula kingi lakini kabohidrati tu kama ugali bila makundekunde, nyama au samaki.

Vyakula vyenye protini nyingi ni

Utaalamu

Protini zilitambuliwa na mwanakemia Msweden Berzelius mwaka 1838.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Protini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA