Chake Chake : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
+ picha + ramani LL
d roboti Nyongeza: sv:Chake Chake
Mstari 41: Mstari 41:
[[en:Chake-Chake]]
[[en:Chake-Chake]]
[[ro:Chake Chake]]
[[ro:Chake Chake]]
[[sv:Chake Chake]]

Pitio la 11:44, 11 Oktoba 2009


Jiji la Chake Chake
Jiji la Chake Chake is located in Tanzania
Jiji la Chake Chake
Jiji la Chake Chake

Mahali pa mji wa Chake Chake katika Tanzania

Majiranukta: 5°14′24″S 39°46′12″E / 5.24000°S 39.77000°E / -5.24000; 39.77000
Nchi Tanzania
Mkoa Pemba Kusini
Wilaya Chake Chake

Chake Chake ni mji mkubwa kwenye kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni makao makuu ya wilaya ya Chake Chake katika mkoa wa Pemba Kusini (South Pemba).

Katika kata tatu za Chachani, Tibirinzi na Wara kuna takriban wakazi 15,000.

Mji umeenea kwenye kilima juu ya hori inayoingia ndani ya kisiwa. Bandari ya Chake Chake haina kina cha kutosha kwa meli hivyo hutumiwa na jahazi au dau ndogo tu.

Kitovu cha mji ni eneo la sokoni penye maduka, hospitali, boma la kale na hoteli ya SMZ. Kando la mji kuna uwanja mpya wa michezo na hospitali mpya.

Uwanja wa ndege wa Wawi uko kilomita saba kutoka mjini upande wa mashariki. Huo ni uwanja wa ndege wa pekee kisiwani ukihudumia ndege ndogo tu.

Chake Chake inasemekana ni mji wa kale lakini hakuna majengo ya kihistoria inayoonekana ila tu boma la kale. Habari zake zimepatikana tangu karne ya 19. Wataalamu huamini ya kwamba umeanzishwa tayari na Wareno karne 4 - 5 zilizopita kwa sababu minara yake yenye umbo la mraba si kawaida katika ujenzi wa Waswahili na Waarabu.

Chini ya mji kuelekea kihori kuna bado mabaki ya boma dogo penye mizinga miwili ya kale.


Viungo vya Nje