Kitenzi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: eu:Aditz
d roboti Nyongeza: nds-nl:Waarkwoord
Mstari 67: Mstari 67:
[[ms:Kata kerja]]
[[ms:Kata kerja]]
[[nds:Verb]]
[[nds:Verb]]
[[nds-nl:Waarkwoord]]
[[nl:Werkwoord]]
[[nl:Werkwoord]]
[[nn:Verb]]
[[nn:Verb]]

Pitio la 00:23, 19 Agosti 2009

Kitenzi ni istalihi ya sarufi kwa maneno yanaotaja matendo kama vile kufanya, kwenda, kulala, kupiga, kuishi na kadhalika.

Lugha nyingi zinatumia vitenzi ingawa kuna pia lugha zisizoweka tofauti kati ya vitenzi na majina.

Kwa Kiswahili kila kitenzi kina shina yake inayobeba maana yake. Mfano: ku-fanya ambamo "fanya" ni shina; kiambishi awali "ku-" ni alama ya aina ya neno yaani kitenzi chenyewe.

Ndani ya shina kuna tofauti kati ya mzizi wa neno "fany" na kiambishi tamati ambacho ni silabi "a".

Mzizi wa kitenzi mwenyewe hubadiliki.

Vitenzi kwa Kiswahili hupokea viambishi mbalimbali vinavyoeleza kwa undani zaidi maana ya matumizi ya neno. Viambishi awali ni silabi vilivyopo mbele ya mzizi na viambishi tamati ni silabi vilivyopo baada ya mzizi.

Viambishi awali vinaweza kutaja

  • nafsi mtenda - ni nani au nini anayetenda na hivi ni silabi ni /u / a upande wa umoja na tu / m / wa upande wa uwingi
  • njeo au wakati - kama tendo linatokea sasa au lilitokea wakati uliopita au litatokea wakati ujao; mifano ni silabi za a pamoja na na kwa wakati wa kisasa, li kwa wakati uliopita na ta kwa wakati ujao.

Viambishi tamani vinaweza kupanusha au kubadilisha maana ya kimsingi ya mzizi wa neno. Mifano ni kimbi-a, kimbi-lia, kimbili-ana, kimbi-za, kimbi-zana, kimbi-liwa.