Mfereji wa Suez : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: war:Kanal han Suez
d roboti Nyongeza: be:Суэцкі канал
Mstari 41: Mstari 41:
[[az:Süveyş kanalı]]
[[az:Süveyş kanalı]]
[[bat-smg:Soeca kanals]]
[[bat-smg:Soeca kanals]]
[[be:Суэцкі канал]]
[[be-x-old:Суэцкі канал]]
[[be-x-old:Суэцкі канал]]
[[bg:Суецки канал]]
[[bg:Суецки канал]]

Pitio la 18:29, 30 Juni 2009

Manowari ikipita katika Mfereji wa Suez
Mfereji wa Suez kutoka angani kati ya Mediteranea (juu) na Bahari ya Shamu (chini)

Mfereji wa Suez (Kiarabu: قناة السويس, qanā as-suways) ni mfereji mubwa nchini Misri.

Mahali pake

Unaunganisha Bahari ya Mediteranea na Bahari ya Shamu hivyo na Bahari Hindi. Mfereji uko upande wa magaribi ya rasi ya Sinai. Urefu wake ni 163 km na upana ni kuanzia 300m.

Unaanza mjini Port Said (Būr Sa'īd) upande wa Mediteranea na kuishia mjini Suez (al-Suways) upande wa Bahari ya Shamu.

Historia

Ilijengwa kati ya 1859 na 1869 na kampuni ya kifaransa.

Kuna mifereji mbalimbali iliyotangulia hapa kuanzia karne ya 14 KK hadi wakati wa Waarabu katika karne ya 8 BK. Lakini yote haikudumu kwa sababu ya matatizo ya kuondoa mchanga mara kwa mara kwa mitambo iliyopatikana zamani. Tena katika mifereji ya zamani ilikuwa serikali ya MIsri tu iliyotaka kurahisisha usafiri na ubebaji wa mizigo.

Tangu kupatikana kwa meli ya kisasa idadi ya meli kati ya Ulaya na Asia iliongezeka sana katika kare ya 19. Zote zilipaswa kuzunguka Afrika yote au kuondoa mizigo na abiria upande wa mediteranea na kuyasafirisha yote hadi Suez. Hivyo ilikuwa jitihada ya kimataifa yaliyoleta mfereji wa kisasa.

Meli ya kwanza ilipita mfereji mpya tar. 17 Februari 1867. Mtungaji muziki Giuseppe Verdi aliandika opera yake Aida hasa kwa nafasi hii.

Umuhimu wa mfereji wa Suez

Mfereji umeharakisha na kurahisisha usafiri kati ya Ulaya, Asia na Afrika ya Mashariki. Zipatao meli 15,000 zinapita kwenye mfereji kila mwaka.

Mafanikio ya mfereji wa Suez yalihamasisha mianzo ya Mfereji wa Panama.

Kutaifishwa kwa mfereji 1956

Mfereji ulikuwa mali ya Compagnie universelle du canal maritime de Suez au ampuni ya mfereji wa Suez na hisa zake zilikuwa mkononi mwa serikali za Ufaransa na Uingereza.

Mwaka 1956 serikali ya Misri chini ya rais Gamal Abdel Nasser ilitaifisha mfereji na tendo hili likasababisha vita ya Suez ya 1956 ambako Uingereza, Ufaransa na Israel zililazimishwa na mataifa makubwa kujiondoa katika Misri baada ya uvamizi wao.