Uprotestanti : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: lmo:Prutestantesim
d roboti Badiliko: bat-smg:Pruotestantėzmos
Mstari 23: Mstari 23:
[[arz:بروتستانتيه]]
[[arz:بروتستانتيه]]
[[az:Protestantlıq]]
[[az:Protestantlıq]]
[[bat-smg:Protestantizmos]]
[[bat-smg:Pruotestantėzmos]]
[[be:Пратэстантызм]]
[[be:Пратэстантызм]]
[[be-x-old:Пратэстанцтва]]
[[be-x-old:Пратэстанцтва]]

Pitio la 05:15, 27 Juni 2009

Uprotestanti ni aina ya Ukristo iliyotokana na Kanisa Katoliki Ulaya Kaskazini katika karne XVI kufuatana na tapo la kidini na la kisiasa maarufu kwa jina la "Matengenezo ya Kiprotestanti". Wahusika wakuu wa tapo hilo ni Martin Luther na Yohane Kalvini.

Asili ya jina

Mwaka 1529, kikao cha Bunge la Speyer (Ujerumani) lilikataza tena uenezaji wa Matengenezo nchini mpaka Mtaguso mkuu utakaporudisha utaratibu ndaniya Kanisa.

Lakini watawala waliomuunga mkono Luther walitoa hati ya pamoja inayoanza na maneno Protestamur, yaani 'Tunapinga'.

Mwaka 1555 Amani ya Augsburg ilipitisha kauli ya kwamba cuius regio, eius religio, yaani kila raia anapaswa kufuata madhehebu ya eneo anamoishi, kadiri ilivyopangwa na mtawala wake, la sivyo ni lazima ahame.

Teolojia

Uprotestanti unagawanyika katika maelfu ya madhehebu tofauti, lakini inawezekana kutambua mambo kadhaa yanayolingana katika yote:

  • kusisitiza Biblia kama msingi wa imani.
  • kusisitiza "wokovu kwa njia ya imani".
  • kusisitiza ukosefu wa binadamu na haja ya damu ya Yesu kama kafara iliyopangwa na Mungu.