Amerigo Vespucci : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: pap:Amerigo Vespucci
Mstari 59: Mstari 59:
[[th:อเมริโก เวสปุชชี]]
[[th:อเมริโก เวสปุชชี]]
[[tr:Amerigo Vespucci]]
[[tr:Amerigo Vespucci]]
[[uk:Веспуччі Амеріго]]
[[uk:Амеріго Веспуччі]]
[[vi:Amerigo Vespucci]]
[[vi:Amerigo Vespucci]]
[[zh:亚美利哥·韦斯普奇]]
[[zh:亚美利哥·韦斯普奇]]

Pitio la 10:31, 25 Juni 2009

Amerigo Vespucci


Amerigo Vespucci (* 9 Machi 1451 mjini Firenze/Italia, + 22 Februari 1512 mjini Sevilla/Hispania) alikuwa mtoto wa tatu wa mwanasheria wa Firenze. Alikua kuwa mfanyabiashara, nahodha na mpelelezi kwenye pwani za Amerika Kusini. Bara za Amerika zilipokea jina kutoka kwake (Amerigo - Amerika)

Amerigo alifanya kazi kwa kampuni ya Medici akatumwa nayo 1491 kwenda Sevilla katika Hispania. Hapa alikutana na Kolumbus akirudi kutoa Amerika. Mwaka 1499 alichukua nafasi yeye mwenyewe na kibali cha akina Medici akajiunga na safari kwenda Amerika kufuata nyayo za safari ya tatu ya Kolumbus kwa kusudi kugundua zaidi ya pwani jinsi Kolumbus alivyoweza. Mbele ya pwani la Guyana (leo: Surinam) aliachana na wenzake akiendelea kuelekea kusini akafika hadi mdomo wa mto Amazonas akiamini ya kwamba amefika Uhindi jinsi ilivyokuwa imani ya kawaida wakti ule.

Katika safari ya pili kwenda Amerika Kusini mwaka 1501 / 1502 alipita mwambao wa Brazil na Argentina hadi Patagonia. Aliporudi aliamini ya kwamba nchi ngàmbo ya Atlantiki si Asia lakini "dunia mpya" au bara jipya. Maandiko yake yalisambaa kote Ulaya na mjiografia Mjerumani Martin Waldseemüller alitumia jina la "Amerika" kwa heshima ya Amerigo alipochora ramani yake ya dunia ya mwaka 1507.