Waraka wa kwanza kwa Wakorintho : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Mstari 46: Mstari 46:
[[hak:Kô-lìm-tô-chhièn-sû]]
[[hak:Kô-lìm-tô-chhièn-sû]]
[[he:האיגרת הראשונה אל הקורינתים]]
[[he:האיגרת הראשונה אל הקורינתים]]
[[hr:Prva poslanica Korinćanima]]
[[hu:Pál első levele a korinthosziakhoz]]
[[hu:Pál első levele a korinthosziakhoz]]
[[ia:Epistola 1 al Corinthios]]
[[ia:Epistola 1 al Corinthios]]

Pitio la 15:39, 22 Juni 2009

Agano Jipya

{

Barua ya kwanza kwa Wakorintho ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira

Kutoka Korintho (Ugiriki) habari za kusikitisha zilimfikia Mtume Paulo akiwa Efeso (pengine mwaka 57): katika Kanisa kulikuwa na shaka kuhusu imani, mafarakano, upinzani wa Wakristo wa Kiyahudi dhidi yake, na makwazo.

Basi mwaka mzima akawa na mahangaiko kwa wafuasi wake wa Korintho akawaandikia walau barua nne au tano, ingawa sisi tunazo mbili tu; pengine sehemu za baadhi yake zimeshonwa ndani ya 2Kor.

Mpangilio

Mpangilio wa barua ya kwanza una salamu na shukrani, halafu hukumu juu ya matatizo ya Wakristo hasa kufarakana (1Kor 1:10-16; 2:1-4:16), kuzini na kushtakiana mahakamani (1Kor 5-6).

Baada ya hapo akaanza kujibu maswali yao mbalimbali: kuhusu ndoa na useja (1Kor 7), nyama zilizotolewa sadaka kwa miungu (1Kor 8:1-11:1), mwenendo katika ibada na karama (1Kor 11:20-33; 12:4-13:13; 14:18-40), na hatimaye ufufuko wa wafu (1Kor 15:1-28,33-49).

Mwishoni kuna maagizo, taarifa na salamu mbalimbali (1Kor 16:1-4).

Madondoo muhimu

Kati ya mambo mengi muhimu, barua hiyo inatunza simulizi la kwanza la karamu ya mwisho ya Bwana Yesu (11:23-25) na kanuni ya imani ya kwanza inayoorodhesha pia matokeo ya Yesu Kristo Mfufuka (15:3-8).


Kiungo cha nje

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili