Erie (ziwa) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Jamii Pennsylvania + Jamii New York
mbegu-jio
Mstari 17: Mstari 17:
* [[Ziwa Ontario]]
* [[Ziwa Ontario]]


{{mbegu-jio}}


{{stub}}


[[Category:Maziwa ya Marekani|Erie]]
[[Category:Maziwa ya Marekani|Erie]]

Pitio la 18:29, 15 Juni 2009

Ziwa Erie (buluu nyeusi) kati ya maziwa makubwa

Ziwa Erie ni moja ya maziwa makubwa ya Amerika ya Kaskazini. Pamoja na maziwa mengine ya Ziwa Superior, Ziwa Huron na Ziwa Ontario liko mpakani kati ya Marekani na Kanada na mpaka huu umepita ziwani.

Ziwa limepakana na Kanada (jimbo la Ontario) upande wa kaskazini halafu na Marekani (majimbo ya Ohio, Pennsylvania, New York na Michigan) upande wa kusini na magharibi. Jina limetokana na kabila la Waerie walioishi hapa kabla ya kuingia kwa Wazungu.

Ziwa Erie hupokea maji yake kutoka Ziwa Huron kupitia mto Detroit. Kuna pia mito mingine inayoishia moja kwa moja ziwani. Maji hutoka kwa nia ya mto Niagara kwenda Ziwa Ontario. Maporomoko ya Niagara yako kati ya maziwa Erie na Ontario.

Vipimo

Ziwa lina urefu wa kilomita 388 na upana mkubwa wa 92 km. Uso wake una eneo la 25,744 km². Kina cha wastani ni 19 m lakini kina kikubwa chafikia 64 m.

Maziwa Makubwa

Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.