Aral (ziwa) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: hif:Aral Sea
d roboti Nyongeza: ug:شور دېڭىز
Mstari 87: Mstari 87:
[[th:ทะเลอารัล]]
[[th:ทะเลอารัล]]
[[tr:Aral Gölü]]
[[tr:Aral Gölü]]
[[ug:شور دېڭىز]]
[[uk:Аральське море]]
[[uk:Аральське море]]
[[ur:بحیرہ ارال]]
[[ur:بحیرہ ارال]]

Pitio la 14:08, 20 Aprili 2009

Meli ya ziwani inayokaa jangwani mahali pa bandari zamani

Ziwa la Aral ((Kikazakhi: Арал Теңізі (aral tengizi), Kiuzbeki Orol dengizi, Kirusi Аральскοе мοре aralskoye more) ni ziwa la Asia ya Kati linalopakana na Kazakhstan na Uzbekistan. Hadi mwaka 1960 lilikuwa na eneo la maji la 68,000 km² lakini limepungua hadi kubaki na 17,160 km² pekee mwaka 2004. Tangu 1987 kupungua kwa maji kulisababisha ugawaji wa ziwa katika sehemu mbili upande wa kazkazini na upande wa kusini ambazo haziungana tena.

Mito mikubwa inayoingia na kubeba maji yake ni Amu Darya na Syr Darya na mito hii ilitumiwa katika mipango ya Umoja wa Kisovyeti kwa umwagiliaji wa mashamba makubwa ya pamba na mazao mengine. Miradi hii iliyoanzishwa katika mazingira yabisi iliendelea kwa miaka 30 hivi hadi kushindikana; maji yamepotea kwa wingi mashambani na katika mifereji kutokana na usimbishaji na kusababisha kupunguza kwa mazao. Kiasi cha chumvi ardhini kiliongezeka sana jinsi ilivyo mara nyingi katika miradi ya umwagiliaji ya nchi za joto na kumaliza rutba ya udongo.

Ziwa halikupokea tena kiasi chake cha maji likapungua. Sehemu kubwa za eneo la ziwa la awali zimekuwa jangwa. Maji yaliyobaki yameharibika kutokana na maji sumu ya viwanda na mbolea nyingi iliyosukumwa kutoka mashamba mitoni halafu ziwani.

Kuna mradi wa kuokoa angalau sehemu ndogo ya kaskazini. Ukuta ulijengwa kwa shabaha ya kuzuia upotevu wa maji katika jangwa la msingi wa ziwa la kale. Uwiano wa maji yamepanda tena katika sehemu hii ndogo.

Kigezo:Link FA

Kigezo:Link FA