Aljeria : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: hif:Algeria
d roboti Nyongeza: mg:Aljeria
Mstari 252: Mstari 252:
[[lt:Alžyras]]
[[lt:Alžyras]]
[[lv:Alžīrija]]
[[lv:Alžīrija]]
[[mg:Aljeria]]
[[mk:Алжир]]
[[mk:Алжир]]
[[ml:അള്‍ജീറിയ]]
[[ml:അള്‍ജീറിയ]]

Pitio la 01:52, 6 Aprili 2009

Aljeria


Algeria (pia: Aljeria ; Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir) au kwa jina rasmi "Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria" ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia.

Ramani ya Algeria

Algeria ni nchi kubwa ya Afrika baada ya Sudan na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara. Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa lugha ya Kiarabu.

Historia

Kwa lugha, utamaduni na historia Algeria ni sehemu ya dunia ya Kiarabu tangu miaka 1300. Nchi imebaki pia na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wa taifa la Waberber ambao kihistoria ni wenyeji asilia.

Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wake na Dola la Roma iliyoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu.

Jiografia

Sehemu kubwa ya nchi ni jangwa Sahara iko kwa upande wa kusini. Asilimia 20 za Algeria katika kaskazini ni nyumbani kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya ni pwani la Mediteranea na milima ya Atlas.

Atlas inapanda hadi kimo cha mita 2,308.

Sahara inaanza kusini ya Atlas na kanda penye manyasi machache halafu inafuata eneo la matuta ya mchango pasipo na mimea yote. Tena kusini yake ni nyanda za juu ambazo ni hasa maeneo ya miamba matupu. Kwenye kusini kabisa kuna milima ya Ahaggar inayopanda hadi mita 2,918.

Mito ya kudumu iko kaskazini tu sehemu za pwani. Mabonde ya mito ya ndani ni pakavu isipokuwa baada ya mvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa.

Hali ya hewa

Kanda la kaskazini lina hali ya hewa inayoathiriwa na Bahari Mediteranea. Hapa halijoto kwenye mwezi wa Agosti ni 25 °C na 12 °C wakati wa Januari.

Kwenye sehemu za juu kuna baridi hata barafu kwenye majira ya Januari lakin i joto ni kali zaidi wakati wa Julai/Agosti.

Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C katika siku moja. Wakati wa joti halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka chini ya °C kwenye saa za usiku.

Mvua ni haba mno kuna miaka mfululizo bila tone moja. Katika milima ya Ahaggar kuna usimbishaji kidogo kutokana na ukungu kwa hiyo miti kadhaa na mimea mingine iko.


Historia

Historia inayojuikana ilianza na Waberber ambao ni wenyeji asilia.

Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani la Mediteranea. Muhimu kati ya miji yao ilikuwa hasa Karthago iliyopanusha utawala wake hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini). Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.

Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walichukua upande wa Roma wakapata uhuru wao kwa muda kidogo lakini wakati wa karne ya kwanza KK Roma ilianza kutawala eneo la Algeria moja kwa moja.

Numidia na Mauretania zilikuwa bustani ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa hapa. Utawala wa Roma ulivurugika aada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja. Jeshi la Kaisari Justiniano I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma ila tu katika karne ya saba uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.

Kuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini baada ya uhamisho wa serikla ya makhalifa kutoka Medina kwenda [Dameski] Waumawiya walikaza jitihada dhidi ya Afrika ya kaskazini. Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha unenezaji. Walipoenea katika Aölgeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti laki ni jeshi lililofuata lilishinda na hadi mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote maana nchi za leo Tunisia, Algeria na Moroko zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Sehemu kubwa ya Waberber walikuwa haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.

Matokeo haya yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.

Historia ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya 1830 na 1962.

Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angalia hapa.

Kwa sasa Algeria inajenga upya umoja wa kitaifa baada ya vita kali ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka 2002.

Wilaya za Aljeria

Kuna vitengo vya utawala 48 vinavyoitwa wilaya.


1 Adrar
2 Chlef
3 Laghouat
4 Oum el-Bouaghi
5 Batna
6 Béjaïa
7 Biskra
8 Béchar
9 Blida
10 Bouira
11 Tamanghasset
12 Tébessa


13 Tlemcen
14 Tiaret
15 Tizi Ouzou
16 Algiers
17 Djelfa
18 Jijel
19 Sétif
20 Saida
21 Skikda
22 Sidi Bel Abbes
23 Annaba
24 Guelma


25 Constantine
26 Médéa
27 Mostaganem
28 M'Sila
29 Mascara
30 Ouargla
31 Oran
32 El Bayadh
33 Illizi
34 Bordj Bou Arréridj
35 Boumerdès
36 El Tarf


37 Tindouf
38 Tissemsilt
39 El Oued
40 Khenchela
41 Souk Ahras
42 Tipasa
43 Mila
44 Aïn Defla
45 Naama
46 Aïn Témouchent
47 Ghardaïa
48 Relizane



Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira