Parokia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
kiungo cha Dominika ni kisiwa
Mstari 1: Mstari 1:
'''Parokia''' ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa [[Kanisa]], ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu ya [[jimbo]] ([[dayosisi]]) unapofanyika uchungaji wa kila siku chini ya [[kasisi]] anayemwakilisha [[Askofu]].
'''Parokia''' ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa [[Kanisa]], ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu ya [[jimbo]] ([[dayosisi]]) unapofanyika uchungaji wa kila siku chini ya [[kasisi]] anayemwakilisha [[Askofu]].


Kiini cha maisha ya parokia ni [[adhimisho]] la[[Ekaristi]] siku ya [[Dominika]], ambapo jumuia nzima ya Kikristo ya eneo husika inakusanyika isikilize [[Neno la Mungu]], imsifu [[Mungu]] na [[kumega mkate]].
Kiini cha maisha ya parokia ni [[adhimisho]] la[[Ekaristi]] siku ya [[Jumapili]], ambapo jumuia nzima ya Kikristo ya eneo husika inakusanyika isikilize [[Neno la Mungu]], imsifu [[Mungu]] na [[kumega mkate]].


==Jina==
==Jina==

Pitio la 22:50, 9 Machi 2009

Parokia ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa Kanisa, ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu ya jimbo (dayosisi) unapofanyika uchungaji wa kila siku chini ya kasisi anayemwakilisha Askofu.

Kiini cha maisha ya parokia ni adhimisho laEkaristi siku ya Jumapili, ambapo jumuia nzima ya Kikristo ya eneo husika inakusanyika isikilize Neno la Mungu, imsifu Mungu na kumega mkate.

Jina

Jina hilo lilianza kutumika katika karne III kutokana na neno la Kigiriki παρоικια (=ujirani) linalotumika katika tafsiri ya Biblia ya Septuaginta kwa maana ya kukaa ugenini.

Katika Sheria za Kanisa Katoliki

Kanuni 515 za Sheria za Kanisa la Kilatini inasema, "Parokia ni jumuia rasmi ya waamini ambayo imeundwa kwa namna ya kudumu ndani ya Kanisa maalumu na imekabidhiwa kichungaji kwa paroko kama mchungaji wake chini ya mamlaka ya Askofu wa jimbo. Ni juu ya Askofu wa jimbo tu kuanzisha, kufuta na kubadilisha parokia; lakini asizianzishe, asizifute wala asizibadilishe sana kabla hajapokea maoni ya Halmashauri ya mapadri. Parokia iliyoundwa kihalali papo hapo ina hadhi ya nafsi ya kisheria".

Katika madhehebu mengine

Mbali ya Kanisa Katoliki, ambalo lina mtandao mkubwa zaidi wa parokia duniani kote, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na Wakristo wengine kadhaa wanatumia muundo huo.