Urithi wa Dunia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Badiliko: jv:Situs warisan donya
Mstari 59: Mstari 59:
[[it:Patrimonio dell'umanità]]
[[it:Patrimonio dell'umanità]]
[[ja:世界遺産]]
[[ja:世界遺産]]
[[jv:Situs Warisan Donya]]
[[jv:Situs warisan donya]]
[[kn:ವಿಶ್ವ ಪರಂಪರೆಯ ತಾಣ]]
[[kn:ವಿಶ್ವ ಪರಂಪರೆಯ ತಾಣ]]
[[ko:세계유산]]
[[ko:세계유산]]

Pitio la 09:19, 3 Machi 2009

Urithi wa Dunia ni maeneo yenye thamani kubwa ya kiutamaduni au kimazingira duniani yanayoangaliwa na shirika la UNESCO. Orodha rasmi la UNESCO lina mahali pa urithi wa dunia wa kiutamaduni na mahali pa urithi wa dunia wa kimazingira.

Mwanzo wa mwaka 2006 sehemu 827 katika nchi 137 zimekubaliwa.

Mwanzo wa jitihada za kuanzisha hifadhi la urithi wa dunia ulikuwa ujenzi wa bwawa la Assuan lililoelekea kuzamisha majengo mbalimbali ya utamaduni wa Misri na Nubia wa kale chini ya maji. Wakati ule UNESCO ilifaulu kukusanya pesa ili hekalu ya Abu Simbel iliweza kuhamishwa mlimani kabla ya kujaa kwa bwawa.

Tangu 1972 kuna mkataba wa kimataifa wa Stockholm kuhusu hifadhi la urithi wa dunia kiutamaduni na kimazingira. Kila mahali panapopendekezwa ili pakubaliwe panahitaji angalau sifa moja kati ya sita zifuatazo:

  • kuwa na thamani ya pekee ya kisanii
  • kuwa na athira muhimu katika eneo fulani au kipindi cha historia
  • kuwa kitu cha pekee kisichopatikana tena au kuwa na umri mkubwa
  • kuwa mfano bora wa kipindi fulani cha historia ya ujenzi
  • kuwa muhimu katika uhusiano na fikra muhimu au watu muhimu wa historia

Kamati ya World Heritage Committee hukutana kila mwaka na kuangalia maombi ya kupokelewa katika orodha ya urithi wa dunia. Kamati inapokea taarifa kuhusu hifadhi na hali ya urithi uliopo tayari orodhani. Kila baada ya miaka miwili orodha inatolewa upya.

Viungo vya nje

Kigezo:Link FA