Utao : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d The file Image:Taoist_priests_officiating_rites_(0).PNG has been removed, as it has been deleted by commons:User:Martin H.: ''File uploaded by commons:User:Nyo have been identified copyright violation''. ''[[m:User:CommonsDelinker|Trans
d The file Image:Taoist_monks_2.PNG has been removed, as it has been deleted by commons:User:Martin H.: ''Files uploaded by commons:User:Nyo have been identified copyright violation''. ''Translate me!''
Mstari 19: Mstari 19:
==Picha za Utao==
==Picha za Utao==


<gallery>
<gallery></gallery>
Image:Taoist monks 2.PNG|Wamonaki wa kitao
</gallery>


== Viungo vya Nje ==
== Viungo vya Nje ==

Pitio la 18:55, 16 Januari 2009

Faili:Huangti.jpg
Kaisari Huang Ti alikuwa mtawala wa China aliyefuata utao
Alama ya Yin-yang ni nembo la Utao

Utao (pia: udao) ni aina ya imani katika nchi ya China inayoitwa wakati mwingine falsafa na wakati mwingine dini.

Asili yake ni katika karne ya 4 KK wakati mzee Laotze alipoandika kitabu cha Tao te king. Mafundisho yake ni msingi wa Utao.

Nembo yake ni alama ya taijitu inayojulikana zaidi kama yin-yang inayoonyesha jinsi gani vinyume ni umoja.

Pamoja na Ukonfusio na Ubuddha ni moja ya imani tatu zilizoathiri na kuumba utamaduni wa China. Mafundisho yake huonekana katika Siasa, uchumi, sanaa, falsafa, fasihi, chakula, tiba, kemia, jiografia na elimu ya vita.

Tao au Dao kiasili ni neno la Kichina la kutaja "njia". Katika Utao imekuwa njia ya kutaja nguvu inayoratibu ulimwengu. Wafuasi wa Utao huamini ya kwamba hakuna maneno ya kibinadamu yanayoweza kueleza tao yenyewe. Kwa hiyo wanaona umuhimu wa kufuata utaratibu wa maisha badala ya majadiliano ya kinadharia. Tao ina nia yake na mtu anatakiwa kwenda sambamba iwezekanavyo na mwendo asilia wa maisha.

Mafundisho yake hukazia sifa za huruma, upole na unyenyekevu.

Watao wanaokazia upande wakidini wanatafuta raha ya milele. Katika imani yao kuna miungu mingi kwenye ngazi mbalimbali ya enzi. Miungu wa juu ni "watatu walio safi".

Wakati wa ukomunisti mkali chini ya Mao Zedong utao uligandamizwa pamoja na dini zote na mahekalu mengi yaliharibiwa. Wamonaki na makuhani walifungwa gerezani, wengine kuuawa na kulazimihswa kuacha kazi yao. Lakini imani iliendelea kwa siri. Leo hii kuna makadirio ya kwamba labda Wachina milioni 80 hufuata tena Utao pamoja na wengine nje ya Jamhuri ya Watu wa China kama huko Taiwan, Singapur na penginepo.

Picha za Utao

Viungo vya Nje