Daraja takatifu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 3: Mstari 3:
Katika [[Ukristo]] zinaitwa '''daraja takatifu''' vyeo vya [[askofu]], [[kasisi]] na [[shemasi]].
Katika [[Ukristo]] zinaitwa '''daraja takatifu''' vyeo vya [[askofu]], [[kasisi]] na [[shemasi]].


Katika [[Kanisa Katoliki]] na ya [[Waorthodoksi]] ngazi hizo tatu zinaunda kwa pamoja mojawapo ya [[sakramenti]] saba ambazo [[Yesu Kristo]]alizianzishwa na kulikabidhi [[Kanisa]] lake.
Katika [[Kanisa Katoliki]] na ya [[Waorthodoksi]] ngazi hizo tatu zinaunda kwa pamoja mojawapo ya [[sakramenti]] saba ambazo [[Yesu Kristo]] alizianzisha na kulikabidhi [[Kanisa]] lake.


Baadhi ya [[Waprotestanti]] wana huduma hizo lakini kwao si sakramenti.
Baadhi ya [[Waprotestanti]] wana huduma hizo lakini kwao si sakramenti.

Pitio la 10:12, 6 Desemba 2008

Askofu anatoa daraja ya upadri akizungukwa na mashemasi

Katika Ukristo zinaitwa daraja takatifu vyeo vya askofu, kasisi na shemasi.

Katika Kanisa Katoliki na ya Waorthodoksi ngazi hizo tatu zinaunda kwa pamoja mojawapo ya sakramenti saba ambazo Yesu Kristo alizianzisha na kulikabidhi Kanisa lake.

Baadhi ya Waprotestanti wana huduma hizo lakini kwao si sakramenti.

Jina

Katika Kigiriki daraja zinaitwa taxeis, na katika Kilatini ordines, kwa sababu waliopewa wanaunda kundi moja.

Ibada ilivyo

Tangu zamani za Mitume mamlaka inashirikishwa kwa tendo la kumwekea mtu mikono kichwani, kufuatana na mfano wa Musa kwa Yoshua katika Agano la Kale.

Tendo hilo linafuatana na sala maalumu ambayo, katika kumuomba Roho Mtakatifu amshukie mhusika, inaweka wazi daraja gani inatolewa.

Anayetoa daraja

Kwa kawaida mwenye jukumu la kutoa daraja takatifu ni askofu wa jimbo (dayosisi), ingawa historia ya Kanisa inasababisha maswali kadhaa juu ya jambo hilo hasa upande wa daraja za chini.

Anayeweza kupewa

Ni imani ya Kanisa Katoliki, ya makanisa ya Waorthodoksi na ya madhehebu mengine kadhaa kwamba daraja zinaweza kutolewa kwa wanaume tu, kwa sababu Yesu aliteua watu wa jinsia hiyo tu awape mamlaka yake ambayo inashirikishwa kwa daraja hizo, na kwa sababu ndiyo mapokeo ya Kanisa tangu mwanzo.

Waprotestanti wanazidi kukubali wanawake katika nafasi zote za uongozi, wakisisitiza usawa wa wafuasi wa Yesu.

Katika Kanisa Katoliki na makanisa ya Waorthodoksi wanaopewa daraja wanaweza wakadaiwa pia hali na ahadi ya useja mtakatifu. Ni hivyo walau kuhusu uaskofu, lakini pengine hata kuhusu upadri.

Hali ya kudumu

Sawa wa sakramenti za Ubatizo na Kipaimara, katika imani ya Wakatoliki daraja takatifu zinamtia mwamini alama isiyofutika ya kikuhani aweze kumtolea Mungu ibada katika liturujia na katika maisha yake yote.

Kwa maana hiyo daraja inadumu ndani ya mtu hata akiacha kutoa huduma au kuasi kabisa.

Vyeo vingine visivyo sakramenti

Katika madhehebu mbalimbali kuna vyeo tofauti na daraja takatifu, ambavyo vilianzishwa na Kanisa kulingana na mahitaji ya mahali na nyakati, kama vile vya Patriarki, Kardinali, Askofu mkuu, Korepiskopo, Paroko, Vartan, Mwenyekiti n.k.

Katika Kanisa Katoliki cheo cha kwanza ni kile cha Papa , ambacho kinategemea na kudai sakramenti ya daraja katika ngazi ya uaskofu kwa sababu ni kukabidhiwa jimbo la Roma kama mwandamizi wa Mtume Petro aliyefia huko.

Imani ya Kanisa hilo ni kwamba cheo hicho, ingawa si sakramenti, ni mpango wa Yesu aliyetaka mitume wake wawe kundi moja chini ya Petro, hivyo waandamizi wao wawe kundi moja chini ya mwandamizi wa Petro, yaani maaskofu wote duniani wawe kundi moja chini ya mkuu wao, askofu wa Roma.