Chai : Tofauti kati ya masahihisho
d roboti Nyongeza: fiu-vro:Tii |
d roboti Ondoa: rw:Icyayi |
||
Mstari 93: | Mstari 93: | ||
[[ro:Ceai]] |
[[ro:Ceai]] |
||
[[ru:Чай]] |
[[ru:Чай]] |
||
[[rw:Icyayi]] |
|||
[[sah:Чэй]] |
[[sah:Чэй]] |
||
[[scn:Tè]] |
[[scn:Tè]] |
Pitio la 05:06, 12 Novemba 2008
Chai ni kinywaji kinachotengenezwa kwa kulowesha majani ya chai (Camellia sinensis) katika maji ya moto. Wakati mwingine hata vinywaji vinavyopatikana kwa kutumia majani ya mimea mingine vinaitwa "chai".
Kwa kawaida chai hunywewa ikiwa moto. Katika Afrika ya Mashariki huungwa maziwa ndani yake pamoja na sukari na viungo vingine. Aina hii ya chai imeenea kutoka Uhindi. Pasipo na maziwa huitwa "chai ya rangi".
Nchi nyingi zina utamaduni wa pekee jinsi ya kutengeneza chai. Wengine hunywa chai bila kitu kingine, wengi hupenda kuongeza sukari tu.
Aina za chai
Majani ya Camellia sinensis huandaliwa kwa njia mbili : kama chai nyeusi na chai ya kijani.
Chai nyeusi hupatikana kwa kukausha majani yake kwanza. Baadye zinavunjwa na kuachwa ziumuke. Hapa kunatokea mmenyuko wa kikemia unaobadilisha rangi na ladha ya majani. Majani hushika joto kutokana na mmenyuko na joto hili halitakiwi kuzidi sentigredi 29. Chai nyeusi hutokea hasa Uhindi, Sri Lanka na Afrika pamoja na Kenya.
Chai ya kijani hutengenezwa kwa kukausha majani mabichi mara moja bila kuyapanafasi ya kuumuka. Chai hii utokea hasa China na Japani.
Chai kama chakula
Neno "chai" hutumiwa pia kwa mlo mdogo. "Karibu chai" humaanisha mara nyingi kumwalika mgeni ale kitafunio hata pasipo na kinywaji chenyewe.
Chai kama hongo
Katika Afrika ya mashariki neno "chai" limetumiwa mara nyingi kudai mahongo. Asili yake ilikuwa ombi: "Naomba pesa kidogo ili nipate kununua chai". Hii imeshafupishwa mara nyingi kwa matanmko mbalimbali kama "naomba chai", "toa chai" n.k. Kwa kawaida mwomba chai atashangaa akipewa kile anachosema kwa sababu anategemea pesa.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |