Kitabu cha Yoeli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: tl:Aklat ni Joel
No edit summary
Mstari 2: Mstari 2:


Hivyo ni pia sehemu ya [[Agano la Kale]] katika [[Biblia]] ya [[Ukristo]].
Hivyo ni pia sehemu ya [[Agano la Kale]] katika [[Biblia]] ya [[Ukristo]].

Kama vitabu vingine vyote vya [[Biblia]], hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa [[Historia ya Wokovu|historia ya wokovu]] ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya [[Ufunuo|ufunuo]] wa [[Mungu]] kwa [[binadamu]].


==Muda wa uandishi==
==Muda wa uandishi==

Pitio la 11:01, 1 Novemba 2008

Kitabu cha Yoeli ni kimoja kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh.

Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Ukristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Muda wa uandishi

Inawezekana kwamba kitabu hiki kilikuwa cha mwisho kuandikwa kati ya vitabu vya kinabii cha Biblia ya Kiebrania (ambamo Kitabu cha Danieli, kilichoandikwa baadaye, hakimo katika kundi la Manabii).

Muhtasari

Katika sura mbili za kwanza, uvamizi wa nzige unaharibu mkoa wote wa Yudea na kuwafanya wenyeji waendeshe liturujia ya toba ambayo iliitikiwa na Mungu kwa ahadi ya kusamehe na kurudisha hali njema.

Katika sura mbili zinazofuata unatabiriwa kwa mtindo wa kiapokaliptiko hukumu ya mataifa na ushindi wa moja wa moja wa Mungu na taifa lake, Israeli.

Mwangwi katika Agano Jipya

Mtume Petro alitaja utabiri wa Yoeli akieleza karama zilizojitokeza siku ya Pentekoste ya mwaka 30 BK kutokana na ujio wa Roho Mtakatifu (taz. Yoe 3:1-5 na Mdo 2:16-21).

Mtume Paulo alitumia utabiri huohuo kuhusu Wayahudi na watu wa mataifa mengine pia (taz. Yoe 3:5 na Rom 10:13).

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.