Kitabu cha Yoeli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
New page: '''Kitabu cha Yoeli''' ni kimoja kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika [[Biblia]...
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:32, 10 Oktoba 2008

Kitabu cha Yoeli ni kimoja kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh.

Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Ukristo.

Muda wa uandishi

Inawezekana kwamba kitabu hiki kilikuwa cha mwisho kuandikwa kati ya vitabu vya kinabii cha Biblia ya Kiebrania (ambamo kitabu cha Danieli, kilichoandikwa baadaye, hakimo katika kundi la Manabii).

Muhtasari

Katika sura mbili za kwanza, uvamizi wa nzige unaharibu mkoa wote wa Yudea na kuwafanya wenyeji waendeshe liturujia ya toba ambayo iliitikiwa na Mungu kwa ahadi ya kusamehe na kurudisha hali njema.

Katika sura mbili zinazofuata unatabiriwa kwa mtindo wa kiapokaliptiko hukumu ya mataifa na ushindi wa moja wa moja wa Mungu na taifa lake, Israeli.

Mwangwi katika Agano Jipya

Mtume Petro alitaja utabiri wa Yoeli akieleza karama zilizojitokeza siku ya Pentekoste ya mwaka 30 B.K. kutokana na ujio wa Roho Mtakatifu (taz. Yoe 3:1-5 na Mdo 2:16-21).

Mtume Paulo alitumia utabiri huohuo kuhusu Wayahudi na watu wa mataifa mengine pia (taz. Yoe 3:5 na Rom 10:13).